Showing posts with label Sports. Show all posts
Showing posts with label Sports. Show all posts

Friday, April 21, 2017

Simba waomba kuandamana Jumanne



Rais wa Simba, Evans Aveva
Klabu ya Simba leo imeandika barua kwenda kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuomba kufanya maandamano ya amani siku ya Jumanne ya tarehe 25 mwezi huu
Imesema lengo ya maandamano hayo ni ili kupeleka ujumbe kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakidai kuwa klabu hiyo imekuwa ikionewa na kutotendewa haki na shirikisho hilo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Rais wa Simba Evans Aveva ambayo imekwenda kwa jeshi la polisi wameomba kufanya maandamano hayo ya amani ambayo yatakwenda mpaka kwa Waziri na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.
Katika taarifa hiyo, Simba inaendelea kusisitiza kuwa klabu hiyo imeendelea kuonewa huku malalamiko yake mengi yamekuwa hayafanyiwi kazi kwa haraka.
Hii ndiyo barua yao.......

Tukio linaloweza kumfanya Ibrahimovic asirudi uwanjani msimu huu


Man United ni miongoni mwa timu zilizochezwa mchezo wake wa marudiano wa robo fainali ya UEFA Europa League dhidi ya Anderletch usiku wa April 20 2017 katika uwanja wake wa Old TraffordMan United walicheza game hiyo na kukutana na upinzani mkubwa uliyopelekea game yao kuongezwa dakika 120.
Man United wamefanikiwa kuondoka na ushindi wa magoli 2-1 magoli ambayo yalifungwa na Mkhitaryan dakika ya 10 na Marcus Rashford dakika ya 107 wakati goli pekee la Anderletch lilifungwa na Hanni dakika ya 32, hivyo Man United kuingia hatua ya nusu fainali kwa aggregate ya magoli ya 3-2.
Hata hivyo Man United wamepata ushindi uliyoambatana na pigo kwa mshambuliaji wao tegemeo Zlatan Ibrahimovic kuumia goti la kulia  na kutolewa dakika ya 91, hivyo kuumia huko kuna hofu kubwa kuwa Zlatan inawezekana akamaliza msimu huu akiwa nje ya uwanja licha ya kuwa haijathibitika bado.

HAYA NDIO MATOKEO YA EUROPA LEAGUE

AET
Besiktas
Lyon *
FT
Genk
Celta Vigo
AET
Manchester United
Anderlecht
AET
Schalke 04
Ajax

KRC Genk ya Samatta imeshindwa kuvunja rekodi ya historia Ubelgiji

Usiku wa April 20 2017 michuano ya robo fainali ya UEFA Europa League iliendelea tena kwa michezo ya marudiano ya robo fainali kuchezwa, timu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilicheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Celta Vigo katika uwanja wake wa nyumbani wa Luminus Arena.
Mchezo huo kati ya KRC Genk dhidi ya Celta Vigo ilikuwa ni mchezo ambao KRC Genk walikuwa na mtihani wa kuvunja rekodi nzito ya Celta Vigo ambapo katika historia hawajawahi kufungwa na timu za Ubelgiji katika mashindano ya UEFA Europa League licha ya kuwa msimu ndio mara ya kwanza ya Genk na Celta Vigo kukutana.
Genk wameondolewa na Celta Vigo katika hatua hiyo kwa kulazimishwa kwa jumla ya magoli 4-3, hiyo ni baada ya leo kutoka sare ya 1-1 kwa goli lilifungwa na Trosand dakika 67 baada ya Sisto kuifungia Celta Vigo goli la uongozi dakika ya 63, lakini Genk walifungwa kwa magoli 3-2 katika mchezo wa kwanza uliyochezwa Balaidos.

Kikosi bora cha wiki cha UEFA Champions League Lionel Messi OUT!!!!

Usiku wa April 18&19 2017 michezo ya robo fainali ya UEFA Champions League msimu wa 2016/2017 ilichezwa kwa michezo minne kuchezwa, michezo hiyo ilichezwa huku tukishuhudia baadhi ya record zikiwekwa kama Kylan Mbappe akiwa mchezaji wa kwanza kushinda michezo minne za kwanza ya mtoano UEFA Champions League.
Wakati Juventus walikuwa ni timu ya tatu kuwahi kuitoa FC Barcelona katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya pasipo kuruhusu kufungwa goli hata moja baada ya Man United na FC Bayern Munich kuwahi kuifanya hivyo, baada ya kujua timu za Atletico MadridJuventusAS Monaco na Real Madrid zimeingia nusu fainali ya Championse League, leo UEFA wametangaza kikosi bora cha wiki.

Thursday, April 20, 2017

ABDI Banda Sasa Huru Kuitumikia Simba..!!!




Beki wa Simba Abdi Banda hivi sasa yupo huru kuitumikia klabu yake ya Simba baada ya leo adhabu yake kutangazwa  kumaliza kutumikia adhabu yake . Mchezaji huyo alifungiwa na Bodi ya Ligi baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar,  George Kavila

Kamati ya nidhamu ilikaa siku ya jana na wakati inakaa tayari mchezaji huyo alikuwa amekosa mechi mbili hivyo kamati ilipitia  na kusikiliza pande zote mbili na kufanya maamuzi kuwa zile mechi mbili ambazo mchezaji huyo alizikosa ndiyo adhabu yake tosha kwa kosa alilofanya.

Awali mchezaji huyo baada ya kufanya tukio hilo ambalo mwamuzi hakuliona, alisimamishwa kucheza ligi kuu kusubiri maamuzi, na akakosa michezo dhidi ya Mbao FC na Toto Africans.

Mchezaji huyo wa Simba ataungana na wachezaji wengine wa klabu hiyo ambao wataingia kambini siku ya Jumapili kujiweka sawa dhidi ya mechi zilizobaki kwenye Ligi Kuu Bara ambazo zinaendelea nchini.

Kikosi bora cha Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017

Leo April 20 2017 PFA wametangaza kikosi bora cha Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017, kikosi hicho ambacho kimetangazwa na PFA wachezaji wa Chelsea na Tottenham Hotspurs ndio wamepata nafasi ya kuingia katika list hiyo ya wachezaji 11.

Tuesday, April 18, 2017

Mbwana Samatta anatajwa kwenda kumrithi Robin van Persie

Headlines za usajili barani Ulaya zimeanza kuchukua nafasi wakati huu ambao Ligi Kuu mbalimbali barani humo zinakaribia kumalizika, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta ameanza kuhusishwa na Fenerbahce ya Uturuki.
Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji ameanza kuhusishwa na club hiyo kutokana na uwezo wake licha ya kuwa maamuzi hayo ya Fenerbahce yanatajwa kushangaza wengi, Fenerbahce kwa sasa wanatafuta mbadala wa mshambuliaji wao Robin van Persie ambaye anaonekana kuchoka.
Samatta ambaye ana umri wa miaka 24 anatajwa kutazamiwa na Fenerbahce kumrithi Robin van Persie aliyewahi kuvichezea vilabu vya Arsenal na ManUnited ya England, wachezaji wengine wanaotazamiwa na Thomas BrunsTheo Bongoda na Ridgeciano Haps.
CHANZO CHA HABARI HII: mwananchi.co.tz

SIMBA SC YALIA NA WIKPEDIA..... SOMA

Ukipitia ukurasa wa Wikipedia na ukatafuta maelezo kuhusu Club ya Simba basi wameelezea kuwa Simba Official Nick Name  yao ni Wamatopeni

Ukurasa huo wa kujuza watu mambo unasomeka hivi:

Wednesday, March 16, 2016

ANGALIA SHABIKI HUYU WA MPIRA JINSI ALIVYOFUNGA NDOA

Mashabiki wa soka ni watu ambao hupenda kufanya vitu kwa ajili ya mapenzi na timu au wachezaji wao, mtu wangu wa nguvu, nimekutana na harusi mbili ambazo huenda zikawa zinashangaza zaidi katika historia ya ushabiki wa soka.
1- Hii inashangaza kwa sababu tumezoea kuona mtu akifunga ndoa, wakati wa harusi huwa anavaa suti au hata suruali ya kitambaa na shati na tai. Lakini kuna shabiki wa soka wa Arsenal alifunga ndoa akiwa kavaa jezi ya Arsenal kuanzia juu hadi chini.
CZBCg0gWkAAdGyf
2- Huyu mwingine yeye alifunga ndoa kawaida tu akiwa kavaa suti na bibi harusi akiwa kavaa shela, sasa stori ni pale wakati ambapo wanaingia ukumbini, baada ya kupigwa wimbo wa kawaida, maharusi waliingia wakiwa na wimbo wa UEAFA, yaani wimbo ambao unapigwa wakati wa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Sunday, February 21, 2016

TETESI ZA SOKA,,,,,ROONEY ATAKIWA KUCHEZEA KLABU YA CHINA,,,STORY ZAIDI IKO HAPA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza na nahodha wa klabu ya Man United Wayne Rooney wiki hii aliingia kwenye headlines baada ya klabu ya wachina ya Shanghai Shenhua kuomba kumsajili kutoka klabu yake ya Man United na kwenda kuanza maisha mapya ya soka nje ya Uingereza kwa mara ya kwanza.
Klabu ya Shanghai Shenhua ambayo ilianza kuiomba Man United kumsajili Wayne Rooney kwa dau la pound milioni 27 mwishoni mwa mwaka 2015, kwa sasa inamuhitaji na ilitaka kuwa inamlipa mshahara wa pound 500,000 kwa wiki,  katika mkataba wa miaka mitatu, mshahara ambao ni mara mbili ya anaolipwa na Man United kitu ambacho kingemfanya Wayne Rooney avune zaidi ya Tsh bilioni 220 kwa kipindi cha miaka mitatu nje ya posho na bonansi za mechi.
rooney
February 20 Wayne Rooney anaripotiwa na Sunday Times kukataa mpango huo wa kujiunga na klabu hiyo ya China. Kama utakuwa unakumbuka vizuri, klabu ya Shanghai Shenhua iliwahi kuwasajili wachezaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba na Nicolas Anelka, Hivyo Rooney kukataa mpango huo wa kujiunga na klabu hiyo unafananishwa sawa Rooney na kukataa zaidi ya Tsh bilioni 220.

Sunday, January 31, 2016

Rais Magufuli 'ampa tano' kwa Samatta

Mwana Samatta baada ya kutambulishwa Genk
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Nahodha wa timu ya Taifa ya Soka Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Samatta, kwa kusajiliwa na timu ya KRC Genk inayocheza ligi kuu ya Ubelgiji, Barani Ulaya.
Katika Salamu hizo kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Moses Nnauye, Rais Magufuli amesema Mbwana Samatta ameijengea heshima Tanzania na kuitangaza kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Rais Magufuli amesema mafanikio ya Samatta kwenda kucheza katika ligi kubwa duniani, kunafungua milango ya wanasoka wengine wa Tanzania kujiunga na timu kubwa duniani, ambako licha ya kujipatia ajira zenye kipato kizuri, kunaiwezesha kuinua soka lake.
Taarifa hiyo imemnukuu Rais Magufuli akisisitiza "Nimefurahishwa na mafanikio anayoendelea kuyapata Mbwana Samatta, nawaomba wanasoka wote Tanzania wayachukue mafanikio haya kama changamoto ya kufanya vizuri na kuzivutia timu mbalimbali za ndani na nje ya nchi"
Aidha, Rais Magufuli amemtaka Mbwana Samatta kuongeza juhudi akiwa katika timu yake hiyo mpya ya KRC Genk, na amemuombea mafaniko mema yeye mwenyewe na timu yake.
Kabla ya kujiunga na timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta alikuwa mchezaji wa timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako alifanya vizuri na kufanikiwa kuwa Mfungaji bora wa ligi ya mabingwa Barani Afrika na pia kutwaa tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

Friday, January 29, 2016

Samatta ajiunga na KRC Genk,Ubelgiji


Image copyrightCAF Online Twitter
Image captionSamatta ajiunga na timu ya Ubelgiji
Sakata ya usajili wa nahodha wa timu ya soka ya Tanzania, Mbwana Samatta inaonekana kukamilika baada ya mshambulizi huyo kukubali kujiunga na klabu ya ubelgiji ya KRC Genk.
Samatta maarufu Samagoal, ameanza safari ya kuelekea Ubelgiji ambapo anatarajiwa kusaini mkataba na klabu hiyo.
Ajenti wa nyota huyo, Jamal Kisongo ametetea hatua ya Samatta kujiunga na Genk licha ya Nantes kutoa donge nono Zaidi ya Genk huku akisema kuwa uamuzi huo ni kwa minajili ya ufanisi wa Samatta.
''Wachezaji wengi waTanzania wanaazimio la kucheza soka Ulaya na naamini fursa hiyo itafika kwani hali ya sasa itafungua milango kupitia Genk''.
Kisongo ameongeza kuwa mkataba huu mpya na Genk utawanufaisha pia wachezaji wa Tanzania kwani makubaliano hayo yataiwezesha klabu hiyo kusaka vipaji zaidi nchini Tanzania.
Samatta ambaye pia ni mchezaji bora wa wachezaji wa nyumbani barani Afrika anatarajiwa kupigania nafasi yake ya kikosi cha kwanza cha Genk.
''Ni muhimu kwa Samatta kuingia na kucheza katika kikosi cha kwanza cha Genk na inatarajiwa hali hio itamwezesha kutimiza ndoto hiyo,'' alisema Kisongo.
Uhamisho wa Samatta unadaiwa kuzua utata baina yake na mmiliki wa klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi kwani Katumbi alichagua Nantes ambayo ilitoa kitita bora zaidi.
-Samatta aliichezea Simba kabla ya kujiunga na TP Mazembe mnamo mwaka wa 2011.
-Aliisaidia TP Mazembe kutwaa taji la vilabu bingwa barani Afrika.
-Alituzwa mchezaji bora Afrika.

Monday, January 11, 2016

ARSENAL WANAAMINI STRIKER HUYU WA AFRIKA ATAWASAIDIA KUTWAA NDOO YA EPL MSIMU HUU

Odion Ighalo
Klabu ya Arsenal inawania saini ya mshambuliaji raia wa Nigeria Odion Ighalo anayekipiga Watford inayoshiriki ligi kuu soka nchini England, katika harakati za kukiongezea nguvu kikosi chao msimu huu ili kuhakikisha wanapata chochote mwisho wa msimu.
Maskauti wa Arsenal chini ya kocha Arsene Wenger wanatafuta mshambuliaji atakayeongeza magoli katika safu yao ya ushambuliaji na kuona kuwa Odion Ighalo zao la Academy ya Manchester United anaweza kufiti katika mahitaji yao.
Odion Ighalo ameshafunga mabao 14 katika mechi 20 ambazo amecheza hadi sasa kwenye raundi ya kwanza ya ligi kuu England
Odion Ighalo ameshafunga mabao 14 katika mechi 20 ambazo amecheza hadi sasa ikiwa ni msimu wake wa kwanza kwenye ligi kuu ya England
Tayari mambo anayoyafanya mshambuliaji huyo kutoka Nigeria yamekua katika rekodi za watu kwani tayari Odion Ighalo ameifungia klabu yake ya Watford magoli 14 katika msimu huu na kuongeza thamani yake katika dirisha hili la usajili.
Lakini Ighalo mwenyewe amekaririwa akisema kuwa itakua ngumu kwake kukataa ofa ya kuichezea klabu aliyokulia ya Manchester United endapo tu kocha Louis Van Gaal atataka huduma ya mshambuliaji huyo ambaye anawataja Dwight Yorke na Andy Cole kama mashujaa wake akiwa Old Trafford.
Aubamechicha
Wakati huo huo klabu ya Arsenal inaangalia uwezekano wa kumnasa mshambuliaji Pierre-Emmerick Aubamayang wa Borussia Dortmund ama mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, mmexico Javier Hernandez ‘Chicharito’.

Mbwana Samatta anatimkia Ubelgiji wakat Thomas Ulimwengu naye akiwa katika mchakato wa kuihama TP Mazembe kutimkia zake Ufaransa kujiunga na Saint Etienne

 Ulimwengu kapombe stars

Mbwana Samatta anatimkia Ubelgiji wakat Thomas Ulimwengu naye akiwa katika mchakato wa kuihama TP Mazembe kutimkia zake Ufaransa kujiunga na Saint Etienne
Baada ya Mbwana Samatta kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Genk ya Ubelgiji na kuikacha klabu yake ya TP Mazembe mshambuliaji mwingine Mtanzania Thomas Ulimwengu ameweka wazi mipango yake ya kuondoka kwenye klabu hiyo ya tajiri Moise Katumbi na kujiunga na Saint Etienne ya Ufaransa.
Ulimwengu ameiambia Goal, amepokea ofa nyingi kutoka Barani Ulaya na anachokifanya kwa sasa ni kuangalia wapi ni sehemu sahihi ambayo itamfanya aweze kungara kama ilivyo TP Mazembe.
“Nampongeza Samatta kwa hatua aliyofikia, anaondoka na mimi niko njiani, nitaondoka Mazembe kuna timu zinanihitaji kama Saint Etienne lakini bado ni suala la kimchakato kidogo,” amesema Ulimwengu.
Ulimwengu amekuwa na mafanikio makubwa kwenye klabu hiyo bingwa Afrika kama ilivyo kwa Samatta, na kutokana na kufanya vizuri kwenye mechi hizo mipango yake ni kucheza Ualya kama ilivyo pacha wake huyo.

Saturday, January 9, 2016

Yaya:'Tuzo la CAF 2015 lilifaa kuwa langu'


Image copyrightGetty
Image captionAubemeyang alishinda tuzo hilo
Kiungo wa kati wa kilabu ya Manchester City Yaya Toure amekasirishwa baada ya kukosa kushinda taji la mwanasoka bora barani Afrika mwaka 2015 lililotolewa na shirikisho la soka barani CAF.
Toure aliyekuwa nahodha wa Ivory Coast wakati timu hiyo iliposhinda kombe la mataifa barani Afrika, alikuwa wa pili nyuma ya mshambuliaji wa Gabon na kilabu ya Borrussia Dortmund Pierre-Emerick Aubemeyang.
''Nadhani hilo ndilo linaloleta aibu barani Afrika'',Aliiambia radio France Kimataifa.''Vitendo kama hivi havifai,lakini tufanyeje''?.
Image copyright
Image captionYaya Toure akimpongeza Aubemeyang aliposhinda tuzo hilo
Toure alishinda taji hilo la CAF kwa miaka minne iliopita na hivi majuzi alituzwa mwanasoka bora barani Afrika mwaka 2015 na shirika la BBC.
Aubemeyang ni mwanasoka wa kwanza kutoka Gabon kushinda taji hilo.

Thursday, September 10, 2015

Maneno ya Diamond Platnumz baada ya kutajwa kuwania tuzo ya MTV Europe Music Awards 2015

.
.
Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz amepata nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika tuzo za MTV Europe Music Awards 2015 zitakazotolewa mwezi October 25, 2015 jijini Milani Italy.
Msanii huyo ambaye ametajwa kuwania tuzo ya MTV Europe Music Awards katika kipengele cha Best African Act, akiongea na ripota wa millardayo.com alisema..‘Kiukweli namshukuru sana mwenyezi Mungu kwasababu najua mimi naamini sio mimi tu watanzania wengi ndoto zenu ni kuomba muziki wetu uweze kutambulika kimataifa sio tu kutambulika bali kupewa heshima kwa taifa letu la Tanzania‘ – Diamond Platnumz
Kwasasa mambo yanaenda vizuri kabisa kwa hiyo kuteuliwa katika tuzo za MTV Europe kwangu ndio mara yangu ya kwanza pia hata kwa Tanzania, namshukuru Mwenyezi Mungu nauzuri tuzo hizo haziangalii chochote kwani zinaangalia kura za watu so naamini muda ukifika basi mashabiki tupige sana kura ili tuweze kufanikiwe kuuleta ushindi nyumbani, nakumbuka mwaka jana walishinda Sauti Sol‘ – Diamond Platnumz
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Diamond Platnumz

HAWA NDIO MAGOLIKIPA SITA BORA DUNIANI

Julio-Cesar
6. Julio Cesar-InterMilan (Brazil)
Tuzo binafsi
Kipa bora wa Serie A mwaka, 2008–09, 2009–10
Kipa bora wa UEFA mwaka : 2009–10
Kipa bora wa kombe la shirikisho mwaka 2013: 
FIFA Confederations Cup Dream Team: 2013
Primeira Liga Best Goalkeeper: 2014–15
 
5. Peter Shilton-Nottingham Forest (England)
Tuzo binafsi.
Kipa bora wa ligi daraja la kwanza mwaka: 1974–75, 1977–78, 1978–79, 1979–80, 1980–81, 1981–82, 1982–83, 1983–84, 1984–85, 1985–86
Mchezaji bora wa wachezaji mwaka: 1977–78
Mchezaji bora wa Nottingham Forest F.C. mwaka: 1981–82
Mchezaji bora wa Southampton F.C mwaka: 1984–85, 1985–86
4. Petr Czech-Chelsea,Arsenal (Jamhuri ya Cech)
Tuzo binafsi
Mchezaji bora wa UEFA Europa chini ya miaka 21: 2002 
Kipa bora wa Ligue 1: 2003–04
Timu bora ya mashindano ya UEFA Euro 2004
Kipa bora wa EPL : 2004–05, 2009–10, 2013–14 
Mchezaji bora wa EPL mwaka: 2004–05, 2013–14
Mchezaji bora wa Czech mwaka: 2005, 2008, 2009,2010, 2011, 2012, 2013 
Mpira wa dhahabu (Jamhuri ya Czech) : 2005, 2006, 2007, 2008, 2010, 2011, 2012, 2013
Kipa bora wa dunia wa IFFHS: 2005 
Kipa bora wa klabu katika michuano ya UEFA: 2005, 2007, 2008
Mchezaji bora wa wa mwezi wa Chama cha soka nchini Uingereza (FA) Premier League Player of the Month: March 2007
Mchezaji bora wa mwaka wa : 2010-11
3. Edwin Van der Sar-Manchester United (Uholanzi)
Tuzo binafsi 
Kipa bora wa mwaka Uholanzi: 1994, 1995, 1996, 1997
Mchezaji bora wa Ulaya : 1995, 2009
Timu ya mwaka ya ESM: 1995–96, 2008–09
Timu ya dunia ya All-Star: 1998 (Mchezaji wa Akiba)
Kiatu cha dhahabu nchini Uholanzi : 1998
Wawania kinyang’anyiro cha FIFA FIFPro World XI : 2006, 2007, 2008, 2009, 2010, 2011
Alikuwepo kwenye kikosi bora cha EPL mwaka : 2006–07, 2008–09, 2010–11 
Mchezaji bora wa mechi michuano ya UEFA: Fainali 2007–08
Alikuwepo katika kikosi bora cha UEFA Euro 2008
Tuzo ya faida ya Barclays : 2008–09
Kipa bora wa EPL : 2008–09
UEFA Club Goalkeeper of the Year : 2009
 
2. Dino Zoff- Juventus (Italia)
Tuzo binafsi
Novemba 2003: Mchezaji bora wa Italy– Alikuwa ni mchezaji bora wa kizazi cha 50 iliyopita, ambapo alichaguliwa na Shirikisho la Soka Ulaya.
Mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or): 1973 (mshindi wa pili).
FIFA Order of Merit: 1984
UEFA European Championship Team of the Tournament: 1968, 1980
Timu ya wachezaji bora wa dunia wa UEFA: 1982
Kipa bora wa dunia wa FIFA: 1982
Tuzo ya mguu wa dhahabu ‘Golden Foot’ “Nguli wa soka”:2004
Mchezaji bora wa Italia “Hall of Fame': 2012
 
1. Manuel Neuer-Bayern Munich (Germany)
Tuzo binafsi 
Alipata tuzo ya medali ya fedha ya Fritz Walter kwa vijana chinya miaka 19 Silver 2005
Tuzo ya Silbernes Lorbeerblatt: 2010
Mchezaji bora wa Ujerumani mwaka: 2011,2014 
Alikuwepo timu ya mwaka ya ESM : 2011–12,2012–13 
Alikuwepo timu ya UEFA Euro mwaka : 2012 
Mchezaji bora wa fainali ya UEFA 2013 kwa upande wa mashabiki
Kipa bora wa dunia wa IFFHS: 2013, 2014
Kikosi bora cha FIFA/FIFPro : 2013,2014
Timu bora ya UEFA mwaka: 2013,2014 
Kikosi cha timu bora ya UEFA cha msimu wa: 2013–14 
Mchezaji bora wa pili wa UEFA: 2014 
Kipa bora wa kombe la dunia mwaka: 2014 
Alikuwepo kwenye kikosi bora cha ‘FIFA World Cup All-Star’ : 2014

MUSIC