Saturday, January 9, 2016

Yaya:'Tuzo la CAF 2015 lilifaa kuwa langu'


Image copyrightGetty
Image captionAubemeyang alishinda tuzo hilo
Kiungo wa kati wa kilabu ya Manchester City Yaya Toure amekasirishwa baada ya kukosa kushinda taji la mwanasoka bora barani Afrika mwaka 2015 lililotolewa na shirikisho la soka barani CAF.
Toure aliyekuwa nahodha wa Ivory Coast wakati timu hiyo iliposhinda kombe la mataifa barani Afrika, alikuwa wa pili nyuma ya mshambuliaji wa Gabon na kilabu ya Borrussia Dortmund Pierre-Emerick Aubemeyang.
''Nadhani hilo ndilo linaloleta aibu barani Afrika'',Aliiambia radio France Kimataifa.''Vitendo kama hivi havifai,lakini tufanyeje''?.
Image copyright
Image captionYaya Toure akimpongeza Aubemeyang aliposhinda tuzo hilo
Toure alishinda taji hilo la CAF kwa miaka minne iliopita na hivi majuzi alituzwa mwanasoka bora barani Afrika mwaka 2015 na shirika la BBC.
Aubemeyang ni mwanasoka wa kwanza kutoka Gabon kushinda taji hilo.

No comments:

MUSIC