Mbwana Samatta anatimkia Ubelgiji wakat Thomas
Ulimwengu naye akiwa katika mchakato wa kuihama TP Mazembe kutimkia zake
Ufaransa kujiunga na Saint Etienne
Baada ya Mbwana Samatta kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea
Genk ya Ubelgiji na kuikacha klabu yake ya TP Mazembe mshambuliaji
mwingine Mtanzania Thomas Ulimwengu ameweka wazi mipango yake ya
kuondoka kwenye klabu hiyo ya tajiri Moise Katumbi na kujiunga na Saint
Etienne ya Ufaransa.Ulimwengu ameiambia Goal, amepokea ofa nyingi kutoka Barani Ulaya na anachokifanya kwa sasa ni kuangalia wapi ni sehemu sahihi ambayo itamfanya aweze kungara kama ilivyo TP Mazembe.
“Nampongeza Samatta kwa hatua aliyofikia, anaondoka na mimi niko njiani, nitaondoka Mazembe kuna timu zinanihitaji kama Saint Etienne lakini bado ni suala la kimchakato kidogo,” amesema Ulimwengu.
Ulimwengu amekuwa na mafanikio makubwa kwenye klabu hiyo bingwa Afrika kama ilivyo kwa Samatta, na kutokana na kufanya vizuri kwenye mechi hizo mipango yake ni kucheza Ualya kama ilivyo pacha wake huyo.
No comments:
Post a Comment