Showing posts with label Sports. Show all posts
Showing posts with label Sports. Show all posts

Sunday, April 14, 2024

ALLY KAMWE ATAMBA NA GUEDE,AHMED ALLY ATIA MBWEMBWE KUIFUNGA YANGA


 


Saturday, April 13, 2024

MAZOEZI YA YANGA TISHIO , AHMED ALLY KILIO TUPU DHIDI YA IHEFU




AHMED ALLY" WANASIMBA WENYE ROHO NGUMU WAJE KWENYE DABI/TUMEPATA MATOKEO MABAYA MFULULIZO
 

Tuesday, August 22, 2017

Emmanuel Okwi aiogopa Yanga

Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, raia wa Uganda, Emmanuel Okwi amefunguka kwa kujitapa kuwa kuelekea mechi dhidi ya watani wa jadi 'Ngao ya Hisani' kesho atahakikisha anaifunga Yanga japo amepatwa na kitete cha kusema ni magoli mangapi ataifunga.
Okwi ameeleza hayo kupitia mahojiano maalum aliyofanya na klabu yake na kusema hawezi kusema ni magoli mangapi atawapachika 'gongo wazi' Yanga kwa kuwa ni klabu ambayo anaiheshimu.

"Game ya Yanga siku zote haiwagi rahisi kwa upande wowote kwa kuwa ni timu yenye wachezaji wazoefu wengi japo na sisi tunawachezaji wazoefu wengi kama wao, tunategemea mchezo wa kesho utakuwa mzuri pia tunamatumaini tutashinda", alisema Okwi.
Pamoja na hayo, Okwi aliendelea kwa kusema "nitahakikisha timu yangu inashirikiana vizuri na wachezaji wenzangu ili tuweze kutoka na matokeo mazuri katika mchezo huo. Siwezi kusema tutawafunga magoli mangapi kwa kuwa ni timu ambayo ninaiheshimu lakini sisi tutajipanga kuhakikisha tunatoka na matokeo mazuri", alisisitiza Okwi.
Okwi ameanza tambwe hizo ikiwa imebakia siku moja kuchezwa kwa mechi ya watani wa jadi siku ya kesho (Jumatano) ambapo mchezo huo umekuwa ukisubiliwa na watu mbalimbali waweze kujua ni nani siku hiyo ataweza kumfunika mwenzake.

Wednesday, July 5, 2017

Zambia yaikamia Taifa Stars Cosafa

Afrika Kusini. Timu ya Zambia inashuka dimbani kesho Jumatano kukabiliana na Taifa Stars kwenye mchezo wa nusu fainali unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali.

Mchezo huo utapigwa mjini Rustenburg, Afrika Kusini huku Kocha Wedson Nyirenda akisisitiza kuwa,  kikosi chake cha Chipolopolo kina matumaini ya kuibuka na ushindi.

Katika mechi mbili kabla ya mashindano hayo, timu hiyo hiyo ilipoteza mchezo mbele ya Msumbiji kwa kufungwa bao 1-0  wakati wa mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon)  na nyingine ikaifunga Afrika Kusini kwenye mechi ya kirafiki.

Hata hivyo, katika mashindano ya Cosafa walishinda mabao 2- 1 dhidi ya Botswana mchezo uliopigwa juzi Jumapili.

Zambia watashuka Uwanjani wakimtegemea mshambuliajia wao, Donashano Malama.

Tuesday, July 4, 2017

John Bocco aitwa Afrika Kusini kujiunga na Taifa Stars

Mshambuliaji mpya wa Simba, John Raphael Bocco ametua nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichopo nchini humo kutokana na mchezaji Mbaraka Yusuph kuwa majeruhi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi ambapo amesema Bocco ameondoka jana nchini kuwafuata wenzake walioko huko kwa lengo la kuchukua nafasi ya mshambuliaji huyo mpya kutoka Azam Fc.

“Mbaraka amepata matatizo kule Afrika Kusini, hali ya hewa ya baridi imemletea matatizo ambayo kwa sasa yanamzuia kucheza hivyo wakati tunatazama hali yake tumemuita Bocco kwanza kuchukua nafasi,” alisema Madadi.

Taifa Stars itashuka dimbani kwa mara nyingine siku ya Jumatano dhidi ya Zambia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya COSAFA inayoendelea kuchezwa huko Afrika Kusini baada ya kuichakaza bao 1-0 Bafana Bafana usiku wa kuamkia leo.

Rasmi John Terry ajiunga Aston Villa

HATIMAYE baada ya kuambiwa hatoongezewa mkataba na klabu aliyoichezea kwa muda mrefu nahodha wa zamani wa Chelsea na England John Terry amesaini kuichezea klabu ya Aston Villa inayoshiriki Championship licha ya kuwa na umri wa miaka 37.

Mmiliki na Mwenyekiti wa Villa Dr Tony Xia alithibitisha kuwasili kwa staa huyo aliyepata mafanikio makubwa akiwa na Chelsea Jumatatu asubuhi, akiandika kwenye Twitter yake: ‘Karibu JT Birmingham city…Aston Villa! #UTV! @AVFCOfficial!’

Kuwasili kwa Terry ambaye alikuwa anawindwa pia na mahasimu wa Villa, Birmingham City kuliwafanya mashabiki wa klabu hiyo kuanzisha group maalumu la WhatsApp kwa ajili ya kumkarubisha.


Alvaro Morata akaribia kutua Man United

UHAMISHO wa Alvaro Morata kwenda Manchester United unakaribia kukamilika baada ya wakala na baba wa mshambuliaji huyo kuhudhuria kikao cha mazungumzo na Real Madrid Jumatatu.

Taarifa nchini Hispania zimesema kwamba Juanma Lopez na Alfonso Morata walikwenda katika ofisi za Real mida ya mchana kukutana na viongozi.

Kikao hicho kilimalizika baada ya muda wa saa moja kwa mujibu wa AS na thamani ya Morata ambaye anatakiwa sana na Manchester United ni Pauni Milioni 70.

Pamoja na hayo, Mashetani hao Wekundu bado hawajaafiki bei ya manunuzi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye amefunga mabao 20 katuika mechi 43 msimu uliopita. 

Taarifa za kikao baina ya Lopez na Real azinazidi kuongeza uwezekano wa uhamisho huo.

Monday, May 8, 2017

Mourinho aigwaya Arsenal game ya leo!

Wakati Manchester na Arsenal wakitarajiwa kukutana jioni ya leo katika Uwanja wa Emirates kwenye mechi ya Premier League, Jose Mourinho amesisitiza kuwa mpinzani wake huyo atafurahi kutokana na yeye kupanga kuchezesha kikosi dhahifu leo
"Yeye (Wenger) ukweli atanifurahia kwa sababu nitabadilisha timu yangu dhidi ya Arsenal," alisema Mourinho. "Tunapaswa kuwa na ubinadamu na kwa wachezaji.
Tunapaswa kuwa na busara na (kuwatumia) kwa akili katika uhusiano kwa hali yetu ya Premier League. Mechi yetu ya mwisho dhidi ya Swansea ilikuwa ya mwisho kwetu kupigania nne-bora, hivyo nitapumzisha wachezaji wangu.
"Hatutakwenda Arsenal kusema “tufungwe tano ama 6-0”. Tunakwenda pale kupigania matokeo.
"Lakini siwezi sasa kuchezesha timu ile ile ambayo ilicheza Hispania na Celta Vigo halafu irudie tena Alhamisi ijayo."

Yanga yarudi kileleni VPL

Tokeo la picha la yanga

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans wametoka vifua mbele baada ya kuwachapa mabao 2-0 wapinzani wao Tanzania Prisons katika mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mabao hayo yote mawili yamepatikana katika dakika 45 za kipindi cha pili cha mchezo huo ambapo ilipofika dakika 71 Amisi Tambwe aliweza kuchungulia nyavu za wapinzani wao kwa mara ya kwanza na kuifanya Yanga kuongoza bao 1-0 na ilipofikia dakika 76 za mchezo Obrey Chirwa aliwainua tena mashabiki wa klabu hiyo kwa kufunga bao la pili na kuifanya timu yake kuibuka kidedea mpaka mpira kuisha.
Kwa matokeo hayo timu ya Yanga imeweza kujiongezea pointi zake 3 na kuifanya kufikia alama 59 sawa sawa na Simba SC.
Katika hatua nyingine Nahodha wa Prisons, Benjamini Asukile amesema pamoja na kufungwa na Yanga bado hawajakata tamaa na Prisons lazima itabaki Ligi Kuu Bara.
“Kuna makosa tulifanya kipindi cha pili na Yanga wakaitumia nafasi hiyo. Lakini tutaendelea kupambana na imani yetu Prisons itabaki ligi kuu”. Alisema Asukile

Sunday, April 30, 2017

MBAO FC YAIVUMUA YANGA

Baada ya Jumamosi ya April 29 Simba kucheza mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Azam FC na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Mohamed Ibrahim dakika ya 48, Yanga leo walishuka dimba kucheza nusu fainali dhidi ya Mbao FC.
Yanga waliingia katika uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Mbao FC katika mchezo huo wa nusu fainali, kabla ya mchezo kumalizika Yanga ndio alikuwa Bingwa mtetezi wa michuano hiyo, kwa bahati mbaya Yanga amevuliwa Ubingwa kwa kufungwa goli 1-0 lililopatikana kwa beki wake Andrew Vincent kujifunga dakika ya 27.
Ushindi wa Mbao FC ambao wanaingia fainali hiyo kwa mara ya kwanza ikiwa ni msimu wao wa kwanza toka wapande kucheza Ligi Kuu, unaifanya sasa kukutana na Simba katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo ya Kombe la FA (ASFC) katika tarehe ambayo itatajwa na TFF.

Friday, April 28, 2017

Zlatan Ibrahimovic amekataa kulipwa mshahara na Man United

Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic amerudi kwenye headlines baada ya maamuzi yake kuandikwa na vyombo vya habari, Zlatan ameripotiwa na mtandao wa dreamteamfc.com kuwa amekataa kulipwa mshahara na Man United.
Zlatan Ibrahimovic atakuwa nje ya uwanja katika kipindi cha miezi 9 baada ya kuumia goti lake la kulia wakati wa mchezo wa marudiano wa  Europa League dhidi ya Anderltch ya UbelgijiZlatan anayelipwa mshahara wa pound 250000 kwa wiki alijiunga na Man United kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Baada ya kujulikana kuwa Zlatan atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 9 Man United walikuwa wapo tayari kuendelea kumlipa mshahara kama kawaida katika kipindi chote cha majeruhi lakini Zlatan amekataa, Zlatan anatarajiwa kurudi uwanja kuanzia mwezi Janury 2018.

Man City na Man United HAKUNA MBABE

eplHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWachezaji wa City na United
Mchezo wa dabi ya jiji la Manchester kati ya Mashetani wekundu wa Man United na Man City umemalizika kwa sare ya bila kufunga mchezo huo ulipigwa katika dimba la Etihad.
Kutoshana nguvu kwa timu hizi kunafanya vita ya kuwania nafasi nne za juu kuendelea kuwa kali City wako nafasi ya nne kwa alama 65 alama moja mbele ya United walioko nafasi ya tano kwa alaam 64.
Man city wakiwa wenyeji wa mchezo huo waliutawala mchezo kwa asilimia kubwa na umiliki wa mpira ukiwa ni asilimia 69 kwa 31.
United walibaki pungufu katika dakika ya 84 baada ya kiungo wake Marouane Fellaini kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu, baada ya kumpiga kichwa Sergio Aguero.Huu ulikua ni mchezo wa 24 kwa Man united wakicheza bila kupoteza msimu huu

Majibu ya klabu ya Yanga kwa Dr Mwakyembe

Kumekuwa Na Mkanganyiko Wa Habari Na Upotoshwaji Wa Taarifa, Ambazo Si Sahihi Kuhusiana Na Yanga Kuchezesha
Kikosi Cha Pili Hapo Jana Dhidi Ya Kombaini Ya Majeshi Katika Uwanja Wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Naomba Kuliweka Jambo Hili Wazi Na Kuondoa Sintofahamu Zisizo Na Msingi Na Pengine Kufunga Mjadala Huu Rasmi.
1.Week End Ya Tarehe 22 Na 23 ,Na Ya 28 Hadi 30 Tff Walitupa Ratiba Ambayo Inaonyesha Hakuna Mchezo Wowote Local League,
Au Fa Cup.Na Ratiba Yetu Ilionyesha Tutacheza Tarehe 22 Fa Cup Dhidi Ya Prisons Tu Kwa Kuwa Ni Kiporo,Na Ukiangalia Ni Wiki Ya Pili Sasa Ligi Haichezwi Kutokana Na Ratiba Ya Chan Yaani Mashindano Ya Kimataifa Ya Caf Kwa Timu Za Taifa Kwa Wachezaji Wa Ndani.
2.Baada Ya Kupata Ratiba Ya Mapumziko Ya Wiki Mbili Bila Michezo Ya Ushindani ,Kama Viongozi Tukaona Si Busara Wachezaji Wakae Bila Michezo Ya Kujipima Nguvu Ili Kuendelea Kujijenga Kuwa Katika Ushindani Muda Wote.
Tukaona Wiki Mbili Ni Nyingi Mno Bora Tupate Michezo Ya Kujipima Nguvu Yaani Friends Matches Katika Majuma Haya Mawili.
Tulipokea Barua Kutoka Arusha Tucheze Mechi Mbili Tarehe 29 Na 30 Dhidi Ya Madini Na Afc,Tukakubaliana Nao Pia Tutaenda Huko.
Tukapokea Barua Ya Dodoma Tucheze Tarehe 26 Tukakubali Pia.
Sasa Tatizo Limekuja Kwa Tff Kufanya Droo Tarehe 23 ,Na Kututaka Tucheze Tarehe 30 Nusu Fainali Ya Fa Cup Ratiba Ambayo Haikuwepo Kabla Ya Hapo ,Sisi Tulikubali Kucheza Michezo Hiyo Tukijua Hakuna Mashindano Yoyote Ndani Ya Tarehe Hizo.
3.Nakiri Kabisa Kuwa Tatizo Limesababishwa Na Ratiba Zisizoeleweka Za Tff Tusingefika Hapo,
Kama Ratiba Ya Tff Ingekuwa Si Kukurupuka Tusingefika Hapo Leo.
Tumecheza Mechi Ya Kiporo Na Prisons Tukashinda Huku Tukiwa Na Majeruhi Wanane Key Players.
Vicent Bossou
Donald Ngoma
Haruna Niyonzima
Juma Abdul
Malimi Busungu
Ally Mustapha
Anthony Mateo
Deus Kaseke
Siku Ya Pili Ratiba Inatoka Tucheze Nusu Fainali,Narudia Tena Nusu Fainali Tucheze Ndani Ya Siku Saba.
Kwa Vyovyote Vile Hata Ingekuwa Vipi ,Kwa Kikosi Tegemezi Cha Wachezaji 18 Tu,Kukichu Kua Na Kwenda Kukipiganisha Katika Michezo Miwili Mfululizo Ambao Mmoja Hauna Tija Kabisa Tena Michezo Hiyo Ipishane Kwa Siku Tatu Tu, Hii Haijawahi Fanywa Na Timu Yoyote Duniani.
4.Kwa Kuliona Hilo Na Kwa Mapenzi Ya Dhati Kabisa Kutoka Mioyoni Mwetu Viongozi Dhidi Ya Wapenda Mpira Wote Wa Mkoa Wa Dodoma Na Maeneo Ya Jirani,Viongozi Kwa Pamoja Sote Tulitafakari Tukasema Kheri Ya Nusu Shari Kuliko Shari Yenyewe.
Kwa Pamoja Tukahamua Kupeleka Timu Ya Kikosi Cha Pili Wakichanganyika Na Wale Wa Kikosi Cha Kwanza Ambao Hawajatumika Muda Mrefu Waungane Na Vijana Hao Kwenda Kuwapa Burudani Wananchi Wa Kanda Ya Kati Dodoma.
5.Nashukuru Timu Ikiongozwa Na Mimi Mjumbe Mkemi,Mjumbe Hashimu Na Mjumbe Siza Imefika Salama Na Bado Ipo Salama Salmin Na Jana Imeonyesha Kiwango Cha Juu Kabisa Na Wale Waliokuwa Hawaamini Waliacha Viti Vyao Na Kushangilia Soka Safi Na Maridadi La Vijana Wa Yanga.
Mpaka Nikawatania Vijana Ni Hali Hii Wangekuja Baba Zao Ndiyo Msingekaa Vitini Muda Wote.
Kwa Machache Ni Hayo Ila Na Peleka Pongezi Kwa Benchi La Ufundi La Yanga B Chini Ya Kocha Shadrack Msajigwa Kwa Kiwango Bora Kabisa Cha Timu Yake Amewapika Vizuri Hakika Hiki Ni Kikosi Hadhina Maridhawa Ya Yanga Hapo Baadae.
Nitakuwa Mchoyo Wa Fadhila Kwa Pato Ngonyani Alikuwa Captain Jana Kiwango Kizuri Hakika Anarudi Sasa.
Yote Katika Mwisho Pongezi Kubwa, Nzuri Sifa Kedekedee Kwa Yusuf Mhilu Mfungaji Bao La Kusawazisha Dhidi Ya Majeshi,Siyo Sifa Hizi Kwa Ajili Ya Goli Tu La Hasha Hakuna Aliyekaa Bila Kutoa Yowe La Furaha Kila Aliposhika Mpira, Huyu Ni Messi Wa Tanzania Kwa Vizazi Vipya Vya Mpira Tanzania.
Mwisho Kabisa Naliomba Shirikisho La Mpira Tanzania (TFF), liwe Linatoa Kalenda Au Ratiba Ambazo Baadae Hazitaleta Mitafaruku Kama Hii Hapo Baadae .
Yanga Oyeee
Daima Mbele
Nyuma Mwiko
Salum Mkemi
Mjumbe Kamati Ya Utendaji Yanga.
Msimamizi Mkuu Wa Idara Ya Habari Na Mawasiliano Yanga.

Wednesday, April 26, 2017

Mbao FC yatangaza kiama kwa Yanga SC

Katika kuelekea hatua ya Nusu Fainali za michuano kombe la Shirikisho (FA), timu ya Mbao FC imeanza kujitapa kwa kusema wapo tayari kwa kuwapokonya ubingwa wapinzani wao Yanga SC siku ya Jumapili huku wakisisitiza kuwa Msuva na Tambwe kuwadhibiti.

Msemaji wa Klabu hiyo, Chrisant Malinzi amesema walikuwa na hamu kubwa ya kukutana na Yanga kwenye FA na kudai wamejiandaa ipasavyo katika safu yao ya ulinzi ambayo wanaamini ndiyo itaweza kuwapa upinzani mkubwa kwa washambuliaji hao.
Tulianza mipango yetu siku nyingi ya kujiandaa katika michuano ya kombe la FA na tulikuwa tukisubiria tu timu ya kupangwa nayo, tulikuwa na kiu ya kucheza na Yanga....Hatuhofii safu ya ushambuliaji ya Yanga kwani na sisi tuna safu nzuri ya ulinzi ya kuweza kuwazuia Msuva na Tambwe, tumejipanga vyema kuhakikisha tunapata nafasi ya kuingia fainali... Lengo letu ni kuona tunafanikiwa kutwaa taji ili kuwakilisha nchi kimataifa". Alisema Malinzi
Pamoja na hayo, timu ya Mbao FC ndiyo itakuwa wenyeji wa mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa alasiri mwishoni mwa Jumaa hili katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Tuesday, April 25, 2017

Tupo fiti kuwavaa Simba Jumamosi - AZAM FC


Nahodha msaidizi wa Azam FC, Himid Mao (Kulia) akiwa na mshambuliaji Mghana, Enock Atta Agyei (Kushoto)
Nahodha msaidizi wa Azam FC Himid Mao amesema, kikosi kizima kinamorali kubwa ya kupata matokeo mazuri kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho (FA) Tanzania Bara dhidi ya Simba mchezo utakaopigwa Jumamosi ya Aprili 29 Uwanja wa Taifa jijini DSM.
Himid amesema, kikosi kipo vizuri na watanufaika na urejeo wa wachezaji muhimu waliokuwa majeruhi.
Morali iko juu, timu ipo vizuri bahati nzuri wachezaji wenzetu karibia asilimia 90 wapo vizuri na wapo fiti na wako tayari kwa mchezo na naamini kocha atakuwa na nafasi nzuri ya kuchagua timu yake ya kwenda kucheza mchezo huo,” amesema Himid Mao
Kiungo huyo anayesifika kwa ukabaji na mwenye mashuti makali, aliongeza kuwa mchezo huo utakuwa mgumu licha ya kufanikiwa kuwafunga mara mbili katika mechi mbili zilizopita.
Usidhani kama mchezo huu wa tatu utakuwa mrahisi kama mara mbili zilizopita tulizoshinda, kwani Simba nayo inajipanga, lakini naamini sisi tutajipanga vizuri zaidi ili kuweza kushinda mechi hiyo inayokuja,” alisisitiza Himid Mao 
Himid ambaye amekulia kwenye timu hiyo kwa takribani miaka tisa sasa, alitoa wito kwa mashabiki wa Azam FC kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuwapa sapoti kwani wao ni sehemu muhimu sana katika timu na uwepo wao utawaongezea nguvu zaidi uwanjani ya kuibuka kidedea.
Kikosi cha Azam FC kipo kwenye maandalizi makali kuelekea mchezo huo, ambapo tayari kimeshaingia kambini hapo jana.

KIMENUKAAAA,HAJI MANARA HATAKI MCHEZO MCHEZO NA MSIMBAZI YAKE

Diamond alijisemea,’Acha Movie Iendelee’. Sinema ya Haji Manara na TFF bado inaendelea. Mkuu huyo wa kitengo cha habari na mawasiliano kutoka Simba ameamua kuvunja ukimya baada ya kushushiwa rungu zito na kamati ya nidhamu ya TFF kwa kuhukumiwa kifungo cha mwaka kutojihusisha na masuala ya soka pamoja na kutakiwa kulipa faini ya milioni tisa.
Kupitia mtandao wa Instagram, Manara ameamua kuandika ujumbe mzito ambao unaashiria kutoridhishwa na adhabu aliyopewa na kamati hiyo.
Salaam… Namshukuru Mungu kwa sasa masuala yangu binafsi ya kifamilia nimeyamaliza.
na naweza sema kitu, kwanza niwape pole nyie kwa haya yaliyonitokea, mm c mtu ninayeamini uonevu c mtu ninayeweza kunyamaza nikiona haki inaporwa, c mtu mwenye moyo dhaifu wa kuogopa kukosoa pale panapopaswa kurekebishwa, na always ntabaki hvyo, Juzi Ijumaa jioni niliambiwa na ofisi yangu imekuja barua toka TFF, ikiniarifu kuna wito wa kunitaka nifike Karume kusikiliza mashtaka dhidi yangu jpili ya jana asubuhi, wakati huo nikiwa zbar kwa masuala yangu ya kifamilia, na ofisi ikaiandikia Tff barua ya kuomba kusogezwa mbele kwa shauri hili hadi jnne ya kesho kwa kuwa ntakuwa nipo Dar.
barua iliwafikia na bnafsi nikaongea na Afred lucas msemaji wao na akanijibu ameipokea yy na imegongwa muhuri na katibu mkuu wa TFF keshaipata, kumbuka hyo ni jioni ya Ijumaaa , Jmosi nikampigia Alfred kuulizia kikao hcho cha kamati kimepangwa lini,akanijibu jtatu ya leo atanijibu, jana tena mkasikia mliyosikia,ni uharaka upi ilionao tff wa kushindwa kunipa haki ya kusikilizwa? natural justice nchi hii haitambuliki!!wahaini na wauaji nao pia husikilizwa,,iweje kwa mtuhumiwa ambae anapigia kelele haki ya mwajiri wake?
kuna hoja dhaifu inajengwa kuwa nilipaswa nijibu bnafsi barua ya Tff , hv ningewezaje kuijibu barua wakati sikuwepo Dar na sikuwa nimeiona na vp klabu yangu isiwe na haki ya kunijibia barua, wakati leo imepokwa haki ya kutokuwa na msemaji? na hv Tff hawajui kuwa mm nilikuwa naongea kwa niaba ya ofisi na klabu yangu?
nikija sababu za kunifungia nimejiuliza ni kaka yangu huyu msemwa aliyekuwa anasoma hii hukumu? nimemuona kwa Millard Ayo, anasoma hukumu ilio kinyume na hati ya mashtaka, hati yao ina makosa mengine na hukumu pia nyingine, ni aina ya hukumu katili zaid kwa vwango vya mpira wetu, ila nawaambia Tff Haji hajawahi kuwa dhaifu wa moyo, anaweza kuwa dhaifu wa kiwiliwili, lakini nna moyo wa Simba, ntapambana kwa kiwango cha juu sana, ntadai haki yangu na ya mwajiri wangu kwa viwango, na ntaziomba kamati zao zipokee rufaa yangu na kukaa kwa uharaka huu walionifanyia, na nipewe haki ya kusikilizwa,nisihukumiwe kishabiki wala kwa chuki, na nawahakikishia kikao kitakachokaa

Saturday, April 22, 2017

LIVE YANGA VS PRISON


MAN UNITED YAPATA PIGO KUBWA MSIMU HUU

Bado wachezaji na benchi zima la ufundi la Man United halitakuamini kwa kilichotokea kwa mshambuliaji wao tegemeo raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic kuwa hawezi kurejea uwanjani kwa siku za karibuni kufuatia jeraha lake la goti alilolipata wakati wa game ya Europa League dhidi ya Anderletch.
Kwa mujibu wa mitandao ya Ulaya hususani ESPN umeripoti kuwa Zlatan Ibrahimovic kufuatia jeraha lake la goti la kulia alilolipata atakaa nje ya uwanja hadi mwezi January 2018, kitaalam Zlatan anaumwa Anterior Cruciate Ligament (ACL), hivyo atalazimika kufanyiwa upasuaji ambao utamchukua muda mrefu kurudi uwanjani.
Jeraha hilo alilolipata Zlatan mastaa wenzake ambao wamewahi kukutana na tatizo hilo wamekuwa wakikaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi 9, mfano Zouma wa Chelsea aliumia katika mchezo dhidi ya Man United 2016 lakini alilazimika kurudi uwanjani baada ya miezi 11.
Hii ni mwaka 2016 Zouma wa Chelsea alipopata jeraha kama la Zlatan lililomuweka nje ya uwanja kwa miezi 11.
Inawezekana huo ndio ukawa mwisho wa Zlatan kuvaa jezi ya Man United kutokana na mkataba wake kuripotiwa kumalizika mwisho wa msimu huu, sasa haijajulikana kama staa huyo aliongeza mkataba na Man United au alikuwa ameingia makubaliano ya awali kama hakuongeza ana asilimia ndogo ya kupewa mkataba mpya akiwa katika majeruhi na akiwa na miaka 35.

Friday, April 21, 2017

TFF yamshtaki Manara Kamati ya Maadili

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), limemfungulia mashtaka ya kinidhamu Msemaji wa Simba Bw. Hajji Manara kwenye Kamati ya Maadili

Mwesigwa (Kushoto) na Manara
Taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo imesema kuwa Manara atapewa mashtaka yake leo na kujulishwa lini na wapi yatasikilizwa.
"Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kila mwanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania analazimika kuheshimu na kufuata kanuni za maadili za shirikisho kama zilivyoainishwa kwenye kanuni zake mbali mbali" Imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Kuhusu aina za wanafamilia wa mpira nchini, taarifa hiyo imetaja kuwa wanafamilia wa mpira wa miguu ni pamoja na wachezaji, makocha, waamuzi, viongozi wa mpira wa ngazi zote na waajiriwa wa taasisi ambazo ni wanachama wa TFF wa ngazi mbalimbali.
Taarifa hiyo imesema kuwa TFF inaendelea kutoa rai kwa wadau wa mpira kuwa pamoja ni kwamba ni haki yao kushauri, kupendekeza, kukosoa lakini yote haya yafanyike kwa staha ili kutunza heshima ya mpira wetu.
Siku Jumanne wiki hii, Mkuu huyo wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara alizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la pointi 3 za Simba na Kagera Sugar, ambapo aliishushia tuhuma nzito TFF hasa viongozi wake wakuu Jamal Malinzi na Celestine Mwesigwa kuwa lengo lao ni kuibeba Yanga na kuikandamiza Simba

MUSIC