Mashabiki wa soka ni watu ambao hupenda kufanya vitu kwa ajili ya mapenzi na timu au wachezaji wao, mtu wangu wa nguvu, nimekutana na harusi mbili ambazo huenda zikawa zinashangaza zaidi katika historia ya ushabiki wa soka.
1- Hii inashangaza kwa sababu tumezoea kuona mtu akifunga ndoa, wakati wa harusi huwa anavaa suti au hata suruali ya kitambaa na shati na tai. Lakini kuna shabiki wa soka wa Arsenal alifunga ndoa akiwa kavaa jezi ya Arsenal kuanzia juu hadi chini.
2- Huyu mwingine yeye alifunga ndoa kawaida tu akiwa kavaa suti na bibi harusi akiwa kavaa shela, sasa stori ni pale wakati ambapo wanaingia ukumbini, baada ya kupigwa wimbo wa kawaida, maharusi waliingia wakiwa na wimbo wa UEAFA, yaani wimbo ambao unapigwa wakati wa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment