Sunday, April 14, 2024

KABILA LENYE MAAJABU YA KUTISHA LINALOPATIKANA TANZANIA


 

ALLY KAMWE ATAMBA NA GUEDE,AHMED ALLY ATIA MBWEMBWE KUIFUNGA YANGA


 


Tuesday, October 17, 2017

Muhubiri aliyesema Mugabe atakufa Leo asema Mungu kasogeza tarehe



Wanasema ni bora ukose kingine chochote lakini sio habari zinazoendelea ulimwenguni sasa hivi ikiwemo hii iliyotokea kwa Rais Mugabe huko Zimbabwe.
Kuna Muhubiri anaitwa Philip Mugadza ambae alitabiri siku kadhaa zilizopita kwamba Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (93) atafariki October 17 2017.
Alisema hicho ni kitu alionyeshwa na Mungu lakini saa kadhaa zilizopita Muhubiri huyo amejitokeza tena hadharani na kusema Mugabe hatokufa tena October 17 kama ilivyopangwa, Mungu ameahirisha mpaka tarehe nyingine.

Philip Mugadza ( picha ya getty images )
Mugadza amenukuliwa akisema “siku tatu zilizopita nimepokea neno kutoka kwa Mungu akisema kifo cha Mugabe kimeahirishwa mpaka tarehe nyingine ambayo haijatajwa, sio kwamba nimekua nikisali ili afe ndio nionekane mkweli bali hili ni neno la Mungu na lazima nilifikishe kama lilivyo
Kwa upande wa Serikali ya Zimbabwe, Waziri wake wa habari alionekana kucheka kuhusu utabiri wa Mugadza na kusema Rais Mugabe mwenyewe ni Mkristo na amekua akimuabudu Mungu, hawezi kuwa na wasiwasi hata kidogo na utabiri unaofanywa na watu.

Harare
Waziri Simon Khaya Moyo amesema Serikali ya Zimbabwe haikupata wasiwasi wowote kwenye utabiri huo na kwamba kazi zimeendelea kama kawaida, itapendeza tu kujua Muhubiri huyo ndio atakufa lini.

ZARI THE BOSS ,AMWAGA CHOZI KWA JAMAA

Kwa wewe unaefatilia habari za mastaa wa bongo na hasa uhusiano wa Mwimbaji Diamond Platnumz na Zari hivi karibuni utakua umeona meeengi yameandikwa na hata Diamond mwenyewe kukiri kuhusu mtafaruku ulioukumba uhusiano huo.
Wengi waliamini kwamba huu ndio unaweza ukawa mwisho wa wawili hawa hasa Zari ambae alionekana kukasirika zaidi baada ya Diamond kukiri kuzaa na Hamisa Mobetto ambapo Zari alifuta picha zote za Diamond pamoja na kutoa kauli zisizopungua 5 zikionyesha dalili za kumalizana na D.
Hata hivyo upepo unaonekana kubadilika baada ya Zari kuanza kuonekana taratibu akiwa na dalili za kurejesha mapenzi yake kwa Diamond Platnumz.
Diamond alipost wimbo mpya wa Harmonize na kutumia mistari hiyo kama dedication kwa Zari ambapo aliandika >>> “We Hodari Mtunza Siri Zangu Hata nikiwa Sina… Hunivumilia na kuamini nitapata… Tafadhali nlindie Roho yangu cha Kukupa sina ila nakuapia Hakiamungu sito kuacha….) Ujumbe wako huo mama☝@zarithebosslady #SHULALA
Baada ya hiyo Zari nae alishukuru na kuweka emoji ya kutokwa chozi kutokana na maneno mazito aliyoyaandika Diamond.


HUYU AMETISHA ,MABOMU ASAFIRISHA KWENYE MADUMU

Askari walimshtukia kijana huyo baada ya kupita kwenye vituo vitatu bila kusimama huku gari hilo likielekea kwenye kambi ya majeshi ya Umoja wa Mataifa kwa spidi kali.
Polisi mjini Kabul wamesema walitumia nguvu kubwa kumsimamisha kwa kulishambulia gari lake kwa risasi.

Wanajeshi wa UN nchini humo wamesema kuwa mabomu hayo yalichanganywa na mbolea na kuwekwa kwenye madumu huku mengine yakiwa kwenye maboksi ya nyanya hii ni baada ya kufanyiwa ukaguzi.

Hata hivyo, mpaka sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lilitoa tamko juu ya tukio hilo.

Kwa mujibu wa UN nchini Afghanistan mamia ya raia wanauawa kila mwezi na makundi ya kigaidi ambapo kuanzia mwezi Januari hadi Septemba watu 1,584 wameshauawa kwenye matukio mbalimbali ya mashambulizi ya kigaidi.

HII KALI NYINGINE,NASSARI KUPELEKA USHAHIDI MWINGINE

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) amewasilisha ushahidi mwingine kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu tuhuma za ununuzi wa madiwani wa Chama hicho.

Madiwani hao nane wa Chadema wamejiuzulu kwa kile walichoeleza kumuunga mkono Rais John Magufuli jambo ambalo Nassari anadai siyo kweli bali walinunuliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya ofisi ya Takukuru Upanga jiji ni humo alisema, " huu ni ushahidi wa tatu na kadri upepelezi ukiwa unaendelea nitaleta mwingine, hii ni kama filamu ya Isidingo."

Nassari alisema alitarajia Rais John Magufuli angewachukulia hatua wateule wake wanaohusishwa katika sakata hilo ili kupisha uchunguzi uweze kufanyika kwa uhuru.

"Tunajiuliza kwa nini Rais hawachukulii hatua DED, DAS au DC wote wa Arumeru kwa kutuhumiwa, watupeleke mahakamani na tungeomba suala hili lichukuliwe kwa uzito wake," alisema Nassari

Naye Mbunge wa Ubungo, Saed Kubunea aliyeongozana na Nassari alisema,"Mimi nimeshiriki hususani kihabari kwani nimewashauri hawa kuutoa kwa umma ili jamii ijue ukweli."

"Tunachojiuliza kwa nini rais yupo kimya, kwa nini mawaziri na viongozi waliotuhumiwa Katika sakata la Almas na Tanzanite aliwasimamisha kwa nini hawa hataki," amehoji Kubenea

Tuesday, August 22, 2017

Tundu Lissu akamatwa na polisi




Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu amekamatwa na polisi leo wakati akitoka Mahakama ya Kisutu na kupelekwa Central Police jijini Dar es Salaam
Afisa habari wa CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha kukamatwa na Tundu Lissu 
"Tumetoka Mahakama ya Kisutu muda huu ambapo Mwanasheria Mkuu wa Chama, Tundu Lissu alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi (uchochezi one) lakini pia alikuwa ni wakili kwenye kesi inayomkabili Yericko Nyerere hapa hapa Kisutu. 
Wakati gari la Lissu likiwa liko getini tayari kwa kutoka, likawa blocked na nyuma ya gari yake pia likasimama gari jingine likiwa na askari polisi wenye silaha, kisha wengine wakamfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na atakiwa kwenda Central Police" alisema Tumaini Makene 
Makene aliendelea kusema baada ya hapo polisi hao walimtaka ashuke kwenye gari yake na kuingia kwenye gari ya polisi kwa ajili ya kwenda Central Police 
Tundu Lissu amekamatwa leo tarehe 22 Agosti 2017 zikiwa zimepita siku tatu toka alipotoa taarifa ya ndege ya Tanzania  'Bombadier Dash Q400' kuzuiliwa nchini Canada kutokana na amri ya mahakama.

MUSIC