Showing posts with label International. Show all posts
Showing posts with label International. Show all posts

Tuesday, October 17, 2017

Muhubiri aliyesema Mugabe atakufa Leo asema Mungu kasogeza tarehe



Wanasema ni bora ukose kingine chochote lakini sio habari zinazoendelea ulimwenguni sasa hivi ikiwemo hii iliyotokea kwa Rais Mugabe huko Zimbabwe.
Kuna Muhubiri anaitwa Philip Mugadza ambae alitabiri siku kadhaa zilizopita kwamba Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (93) atafariki October 17 2017.
Alisema hicho ni kitu alionyeshwa na Mungu lakini saa kadhaa zilizopita Muhubiri huyo amejitokeza tena hadharani na kusema Mugabe hatokufa tena October 17 kama ilivyopangwa, Mungu ameahirisha mpaka tarehe nyingine.

Philip Mugadza ( picha ya getty images )
Mugadza amenukuliwa akisema “siku tatu zilizopita nimepokea neno kutoka kwa Mungu akisema kifo cha Mugabe kimeahirishwa mpaka tarehe nyingine ambayo haijatajwa, sio kwamba nimekua nikisali ili afe ndio nionekane mkweli bali hili ni neno la Mungu na lazima nilifikishe kama lilivyo
Kwa upande wa Serikali ya Zimbabwe, Waziri wake wa habari alionekana kucheka kuhusu utabiri wa Mugadza na kusema Rais Mugabe mwenyewe ni Mkristo na amekua akimuabudu Mungu, hawezi kuwa na wasiwasi hata kidogo na utabiri unaofanywa na watu.

Harare
Waziri Simon Khaya Moyo amesema Serikali ya Zimbabwe haikupata wasiwasi wowote kwenye utabiri huo na kwamba kazi zimeendelea kama kawaida, itapendeza tu kujua Muhubiri huyo ndio atakufa lini.

HUYU AMETISHA ,MABOMU ASAFIRISHA KWENYE MADUMU

Askari walimshtukia kijana huyo baada ya kupita kwenye vituo vitatu bila kusimama huku gari hilo likielekea kwenye kambi ya majeshi ya Umoja wa Mataifa kwa spidi kali.
Polisi mjini Kabul wamesema walitumia nguvu kubwa kumsimamisha kwa kulishambulia gari lake kwa risasi.

Wanajeshi wa UN nchini humo wamesema kuwa mabomu hayo yalichanganywa na mbolea na kuwekwa kwenye madumu huku mengine yakiwa kwenye maboksi ya nyanya hii ni baada ya kufanyiwa ukaguzi.

Hata hivyo, mpaka sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lilitoa tamko juu ya tukio hilo.

Kwa mujibu wa UN nchini Afghanistan mamia ya raia wanauawa kila mwezi na makundi ya kigaidi ambapo kuanzia mwezi Januari hadi Septemba watu 1,584 wameshauawa kwenye matukio mbalimbali ya mashambulizi ya kigaidi.

Wednesday, May 10, 2017

'Grotesque actions' in Penn State fraternity hazing death

Timothy Piazza (c) is seen in this undated photo.Image copyrightABC
Image captionFraternity members waited 12 hours before calling police to help Timothy Piazza (C)
The lawyer for the family of a student who died after falling down stairs during a fraternity initiation has called the group's actions "grotesque".
Timothy Piazza, 19, died in February after he became drunk during a "pledge" event for a fraternity, which is a social club for male students.
Mr Piazza, who was left unconscious for hours, suffered internal injuries before he died in hospital.
Prosecutors charged 18 students at Penn State University over his death.
The charges came after months of a grand jury investigation, which included video from surveillance cameras, testimony and phone records from Mr Piazza's final hours inside the fraternity house.
The report concluded that there was an attempt to conceal evidence of hazing - the initiation ceremony - and underage drinking after Mr Piazza was in hospital.

Syria war: US to arm Kurds in battle for Raqqa

A member of the US-backed Syrian Democratic Forces monitors the town of Tabqa, on April 30, 2017Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionThe SDF is pressing IS back in the key city of Tabqa
US President Donald Trump has approved supplying weapons to Kurdish forces fighting so-called Islamic State (IS) in Syria, the Pentagon says.
Kurdish elements of the Syrian Democratic Forces (SDF) would be equipped to help drive IS from its stronghold, Raqqa, a spokeswoman said.
The US was "keenly aware" of Turkey's concerns about such a move, she added.
Turkey views the Kurdish rebels as terrorists and wants to stop them taking more territory in Syria.
The SDF, which comprises Kurdish and Arab militias, is already being supported by elite US forces and air strikes from a US-led coalition.
The group is currently battling IS for control of the city of Tabqa, an IS command centre just 50km (30 miles) from Raqqa.
A Pentagon source told the BBC the equipment would include ammunition, small arms, machine guns, heavy machine guns, construction equipment such as bulldozers and armoured vehicles.
The source added that the US would "seek to recover" the equipment afterwards.

Analysis: Gary O'Donoghue, BBC News, Washington

The US believes the Kurdish fighters - known as the YPG - will be essential to the city's downfall.
The Pentagon sees them as the most disciplined and organised of the anti-IS groups but Turkish opposition has meant Washington has had to tread a fine line.
The imminence of the fight for Raqqa means delay is no longer an option and the Kurds will be getting a range of equipment.
US sources say they have received assurances from the Kurds that they will leave Raqqa to be governed by Syrian Arabs after the battle.
Turkey's President Erdogan is due in Washington next week - he will not be a happy visitor.

No timeline has been given for when the weapons would start to be supplied.
"We are keenly aware of the security concerns of our coalition partner Turkey," said Pentagon spokeswoman Dana White, who is travelling with US Defence Secretary Jim Mattis in Lithuania.
"We want to reassure the people and government of Turkey that the US is committed to preventing additional security risks and protecting our Nato ally."
Turkey sees the Syrian Kurds as an extension of the PKK separatist group inside Turkey which has been designated a terrorist organisation by the US and EU.

Monday, May 8, 2017

Wizi wa Punda tishio Kenya, ngozi yake ndio kitu pekee Wezi wanachukua

CITIZEN TV ya Kenya imeripoti taarifa ya wizi wa punda uliokithiri huko Turkana kiasi kwamba hata Wakazi wenyewe wamejawa na hofu na kisa kikiwa ni kuuzwa kwa ngozi ya punda hao.
Biashara ya kuuzwa ngozi ya punda inadaiwa kuwa imeletwa na Wachina na kufanya ngozi ya mnyama huyo kupanda thamani hadi shilingi za Kenya 10,000 ambazo ni zaidi ya shilingi laki mbili za Tanzania huku Punda mwenyewe akiuzwa Ksh 5000 (laki moja na elfu nane ya Tanzania).
Wanasema baada ya Wachina kuinunua ngozi hiyo husafirishwa na kwenda kutumika kwenye kutengeneza dawa inayotibu magonjwa mbalimbali kwenye mwili wa binadamu.
...>>>”Unaweza nunua punda kwa elfu 5 au sita na ukauza ngozi kwa Elfu 10 hali hiyo ikaleta thamani ya Punda na ndiomaana wezi wanaiba Punda na kumchuna ngozi ili aje auze ngozi peke yake” – Joseph Losuru 
“Tuliona kwenye media za Nigeria kuwa Punda wameisha lakina na hapa kwetu pia Punda wameanza kuisha” – Lokwale Anton Mfugaji

Friday, April 28, 2017

Meli ya kijasusi ya Urusi yazama Uturuki

Meli ya Liman ikipitia mlango wa bahari wa Bosphorus mwezi OktobaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli ya Liman ikipitia mlango wa bahari wa Bosphorus mwezi Oktoba
Meli ya kijasusi ya Urusi imezama baharini katika pwani ya Uturuki baada ya kugongana na meli ya kubeba mizigo, maafisa wa uchukuzi wa baharini wa Uturuki wamesema.
Wote waliokuwa kwenye meli hiyo wameokolewa.
Urusi awali ilikuwa imethibitisha kwamba meli ya Liman, ambayo ni sehemu ya kundi la meli za taifa hilo katika Bahari Nyeusi ilikuwa imepatwa na hitilafu na kwamba juhudi za kuizuia kuzama zilikuwa zinaendelea.
Chanzo cha kugongana kwa meli hizo hakijabainika lakini kulikuwa na ukungu mwingi eneo hilo.
Meli hiyo ya kijasusi iligonga meli yenye bendera ya Togo ambayo ilikuwa ikisafirisha mizigo, vyombo vya habari Uturuki vinasema.
Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildirim amezungumza na mwenzake wa Urusi Dmitry Medvedev, na kumueleza masikitiko na huzuni yake kutokana na ajali hiyo, duru katika afisi ya waziri mkuu huyo wa Uturuki zimenukuliwa na shirika la habari la Reuters.
Kundi la Meli za Urusi Bahari Nyeusi (BSF) hupitia mlango wa bahari wa Bosphorus Strait kuelekea bahari ya Mediterranean, ambapo hushiriki katika harakati za kijeshi Syria.
Meli hiyo ya Urusi ilikuwa na watu 78 ambao waliokolewa wote.
Ramani
Meli hiyo iligongana na meli ya Youzarsif H takriban 29km kutoka mji wa Kilyos kaskazini mwa mji wa Istanbul.
Haijabainika iwapo meli hiyo ilikuwa inaelekea mlango wa bahari wa Bosphorus wakati huo.

Venezuela kujiondoa kwenye umoja wa OAS

Nchi ya Venezuela imetangaza kujiondoa katika shirika la umoja wa mataifa ya Marekani Kusini (OAS ) kwa madai kuwa, nchi zilizopo ndani ya jumuiya hiyo zinaingilia masuala ya ndani ya nchi yao.
Akiongea na kituo cha runinga cha taifa (VTV), Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Delcy Rodriguez amesema, “Katika OAS, tulitangaza kwamba hatua hizi za usumbufu, zimeegemea upande mmoja, haramu.Tutachukua hatua za haraka za kuandaa barua kwa OAS na kuelezea ni ya kujiondoa kwa Venezuela kwenye huu umoja.”
“Kesho, kama alivyotaka Rais Nicolas Maduro, tutawasilisha barua ya kujiondoa katika umoja wa OAS na tutaanza hatua hizo ambazo zitachukua miezi 24,” ameongeza.
Watu wapatao 30 wamefariki dunia katika maandamano yanayoendelea nchini humo kwa takribani wiki ya tatu sasa,wakimtaka rais Nicolas Maduro kujiuzulu kutokana kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo jambo lililosababisha upungufu mkubwa wa chakula.

US: Mfumo wa kujilinda ''utamuamsha'' rais wa K. Kaskazini

Upelekaji wa mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini ulipingwa na waandamanajiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionUpelekaji wa mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini ulipingwa na waandamanaji
Mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa Marekani unaowekwa nchini Korea Kusini utaanza kufanya kazi katika siku chache zijazo, jeshi la Marekani limesema.
Mfumo huo wa Thaad umetengezwa kuilinda Korea Kusini na majeshi ya Marekani yaliopiga kambi nchini humo dhidi ya vitisho vya Korea Kaskazini.
Vifaa vya mfumo huo vilipelekwa katika taifa hilo siku ya Jumatano, Admirali Harry Harris ambaye ni ni kamanda wa eneo la Pacific alisema kuwa Thaada itaanza kufanya kazi katika siku chache zijazo ili kuiinda Korea Kusini dhidi ya vitisho vya jirani yake Korea kaskazini.

Marekani kuimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini

Taifa la Korea kaskazini limekuwa likitoa picha kuhusu zoezi la kijeshiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionTaifa la Korea kaskazini limekuwa likitoa picha kuhusu zoezi la kijeshi
Mamlaka ya rais Donald Trump imewaelezea maseneta wote 100 wa bunge la taifa hilo kuhusu tishio la Korea Kaskazini na kubaini mikakati ya kuishinikiza Pyongyang kupitia vikwazo vya kiuchumi na vile vya kidiplomasia.
Lengo ni kuilazimu Korea Kaskazini kusitisha mpango wa makombora ya masafa marefu pampja na ule wa Kinyuklia.
Mwandishi wa BBC mjini Washington anasema kuwa mkakati muhimu pia utakuwa kuirai China kuishinikiza Pyongyang.
Maseneta wa Marekani walielezwa na mamlaka ya rais Trump kuhusu tishio linaloletwa na Korea KaskaziniHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMaseneta wa Marekani walielezwa na mamlaka ya rais Trump kuhusu tishio linaloletwa na Korea Kaskazini
Seneta mmoja alisema kuwa habari hiyo kuhusu Korea Kaskazini ilikuwa muhimu sana.
Taarifa iliotolewa kwa niaba ya wizara ya Ulinzi na ile ya kigeni ilisema kuwa Marekani bado itaendelea na mazungumzo lakini imejiandaa kujitetea pamoja na washirika wake.

Tuesday, April 18, 2017

Kifahamu Kikosi Hatari Duniani cha Marekani cha U.S.A Navy 'Seal' Ambacho Tayari Rasmi Kimeshatua Ndani ya Ardhi ya Korea Kaskazini kwa Ajili ya Kuanza Vita..!!!


Yumkini jaribio la mzee wa kiduku limeshtua sana Marekani ambapo sasa ni rasmi Kikosi hatari cha Makomandoo wa Kimarekani ambacho ndicho "The Most Feared Force" katika ulimwengu huu cha US NAVY SEAL inasemekana tayari kiko katika Peninsula ya Korea tangu Jana usiku kikitokea jimbo la Florida nchini Marekani. 

Hiki ni kikosi hatari zaidi duniani ambacho kazi yake ni kufanya operations ambazo ni hatari zaidi mno na za mwisho. US Navy Seal ni mjumuisho wa makomandoo hatari zaidi wanaotumia ujuzi wa hali ya juu na wenye mafunzo ya kitaalamu zaidi kuliko makomandoo wengine wa majeshi yote ya kimarekani. 

Makomandoo hawa ni wale tu wenye uzoefu wa hali ya juu wa kupambana popote pale iwe angani, ardhini au majini, na katika hali yoyote ile iwe barafu, mvua au jua. Na ndio maana ya neno SEAL ambayo kirefu chake ni Sea, Air and Land. 
Kikosi hiki cha US Navy Seal hutumika baada ya makomandoo wengine wa majeshi tofauti ya marekani kusoma Jiografia ya sehem husika, ramani ya ngome za adui na silaha zake then Raisi wa Marekani hutoa ruhusa ya NAVY SEAL kutumika kumalizia Operation. Baadhi ya majukumu/kazi za Navy Seal ni Direct Operations (kama wanavyotaka kumfanyia North Korea), Strategic Special Missions (kama walivyofanya kwa Osama), Hostage Rescue (kama walivyofanya miaka ya nyuma kuwaokoa Ma-Intelligensia wa Kimarekani waliotekwa Iran) na Foreign Internal Defence. 

Mpaka sasa Navy Seal ina jumla ya Makomandoo 8985 ambao ni hatari mno na wenye roho za kinyama. Makomandoo hawa huwa wapo kwenye mazoezi makali ya special operations na trainings ngumu muda wote huko Virginia, Marekani. Mara chache sana Navy Seal huwa Recruited kwenda CIA kufanya kazi za Kiintelligensia wanapotakiwa. Makamu wa Rais wa Marekani Bwana Pence yuko Korea Kusini na inasadikika ujio wake umeambatana na NAVY SEAL waliojichimbia katika Nyambizi zisizoonekana katika pwani ya Korea..

HAKUNA UWOGA TENA ,KOREA KASKAZINI YA JIPANGE KUIPIGA MAREKANI...SOMA HAPA UJUE ZAIDI

KIONGOZI wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameanika kikosi chake maalumu cha kijeshi kwa mara ya kwanza mwishoni mwa wiki hii, kama hatua ya makusudi ya kumwonesha Rais wa Marekani Donald Trump uwezo wake kijeshi.

Kikosi hicho chenye askari waliofunzwa barabara kilipita mitaani jijini hapa Jumamosi wakiimba nyimbo za kizalendo huku wakiwa wamekumbatia bunduki zao zenye uwezo pia wa kurusha mabomu. 

Askari hao wanaosemekana kuwa na vifaa bora vya kivita ndani ya Jeshi la Watu wa Korea, walivalia pia miwani ya kuonea usiku iliyofungwa kwenye kofia zao za chuma huku bunduki zao zikining’inia vifuani.

“Mara tu Kamanda Mkuu Kim Jong Un atakapotoa amri, watasonga mbele kwa lengo la ‘kuuchoma mkuki moyo wa adui kwa kasi ya radi juu ya Mlima Paektu (kilele kirefu kuliko vyote nchini)’,” mtangazaji wa televisheni ya Taifa alisikika akitangaza.

Kujitokeza kwa kikosi hicho kwenye sherehe za Siku ya Jua mwishoni mwa wiki, kulikuja huku kukiwa na msuguano na Marekani na Rais Trump ambaye amekataa kukanusha mpango wake wa kuishambulia Korea Kaskazini kabla Rais Kim  hajabonyeza kiwambo cha kufyatulia makombora ya nyukilia.

Vikosi maalumu nchini viko tayari kulinda nchi hii dhidi ya majeshi ya Marekani, ambayo yanafanya mazoezi ya kumng’oa madarakani Kim mara mapigano yatakapoanza, mchambuzi wa shirika la habari la Yonhap nchini anadai.

Taarifa ya makao makuu ya Jeshi la Marekani – Pentagon, iliwaelezea wanajeshi hao wa Korea Kaskazini kama miongoni mwa waliopewa mafunzo mazuri, wenye vifaa bora, wanaolishwa vizuri na wenye motisha ya hali ya juu ndani ya Jeshi la nchi hii, CNN iliripoti.  

Ilisema kikosi hicho kisiochoonekana mara kwa mara, kinachosemekana kuendesha operesheni za siri nchini, kinaonekana kuandaliwa kwa ajili ya operesheni nzitonzito na kujilinda dhidi ya mashambuilizi kutoka nje.

Taarifa hiyo inaendelea kusema, kwamba vikosi hivyo maalumu huendesha mambo yao katika vitengo maalumu, ikiwa ni pamoja na utambuzi, mashambulizi ya angani na ya majini, makomando na utaalamu mwingine wa kijeshi.

Ilibasihiri pia, kwamba Korea Kaskazini imedhamiria kuendesha mapigano ya masafa marefu, ikitumia makombora ya nyukilia yenye uwezo wa kuishambulia Marekani moja kwa moja. 

Matumizi ya Bangi Kuidhinishwa KENYA


ZAIDI ya Wakenya 1,400 wanaunga mkono ombi la kutaka kuidhinishwa kwa matumizi ya mmea wa bangi baada anayewasilisha hoja hiyo kuwawasilisha ombi lake mbele ya bunge la seneti.

Iwapo ombi hilo la mtafiti Gwada Ogot litaidhinishwa haitakuwa haramu kupanda ama hata kuuza bangi nchini Kenya.

Gwada Ogot anasema kwamba matumizi ya kiafya pamoja na utumizi wa mmea huo viwandani unaojulikana kwa jina la sayansi kama Cannabis sativa una faida nyingi.

Anasema kuwa matumizi ya mmea huo yataimarisha hali ya uchumi.

Sheria ya Kenya inapiga marufuku utumizi wowote wa bangi na kwamba mtu yeyote atakayepatikana akitumia dawa hiyo atashtakiwa kwa uhalifu.

Ogot anaomba bangi kuondolewa miongoni mwa orodha ya vitu haramu na kutaka sheria mpya kuanzishwa ili kuweka bodi simamizi ya utumizi wa mmea huo.

Monday, April 17, 2017

KAMA ULIKUWA HUJUI , UPINZANI UNATISHA NCHINI UTURUKI..SOMA HAPA UJUE ZAIDI

Wafuasi wa upinzani watokea mitaani mjini Istanbul wakipiga sufuriaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWafuasi wa upinzani walitokea mitaani mjini Istanbul wakipiga sufuria
Chama kikuu cha upinzani Uturuki kimesema kuwa kitapinga matokeo ya kura ya maoni baada ya rais Recep Tayyip Erdogan kushinda kura ya kumuongezea mamlaka.
Chama cha Republican People Party (CHP) kinapinga uhalali wa matokeo hayo yaliyokaribiana sana na kusema kulikuwa na kasoro nyingi.
Upande wa rais Recep Tayyip Erdogan uliokuwa unatetea kuwe na rais mwenye mamlaka makuu ulipata ushindi kwa kuzoa asilimia 51 ya kura zilizopigwa.
Ushindi huo ulipokewa kwa sherehe na pia maandamano nchini humo.
CHP kimekataa kukubali matokeo ya ushindi wa Ndio na kimeitisha kurudiwa kwa kura asilimia 60, wakikashifu uamuzi wa kupitisha kura ambazo hazikupigwa muhuri kama halali hadi pale zitakapokataliwa.
Mitatu kati ya miji mikubwa nchini Uturuki - Istanbul, Ankara and Izmir - yote zilipiga kura ya La wakipinga marekebisho katika katiba.
Wafuasi wa upinzani wametokea mitaani mjini Istanbul wakipiga sufuria - utamaduni wa tangu jadi wa maandamano - huku wakiandamana wakipiga kelele.
Wafuasi wa bwana Erdogan walisherehekea wakipeperusha bendera.Haki miliki ya pichaEPA
Image captionWafuasi wa bwana Erdogan walisherehekea wakipeperusha bendera
Wakati huo huo, wafuasi wa Bw Erdogan walisherehekea wakipeperusha bendera, huku rais wao akiwasifu kwa "uamuzi wao wa kihistoria" ambao utaendelea kumuweka madarakani hadi 2029.
Huku asilimia 99.97 ya kura zikiwa zimehesabiwa, kampeni ya Ndio ilishinda kwa asilimia 51.41 ya kura zilizopigwa, huku La ikichukua asilimia 48.59.
Kando na hayo, watu watatu walipigwa risasi na kufa nje ya kituo cha kupigia kura katika mkoa wa kusini mashariki mwa Diyarbakir, katika mzozo kuhusu upigaji kura.
Akiongea kuhusu matokeo ya Jumapili, Tume ya Ulaya ilitoa taarifa ikimshawishi bwana Erdogan kuheshimu ukaribu wa kura na kutafuta njia mwafaka ya upatanisho ikikusudiwa athari kwa marekebisho ya katiba.
Msukumo wa rais Recep Tayyip Erdogan kuwa na rais mtendaji ilishinda na zaidi ya kura asilimia 51.Haki miliki ya pichaADAM BERRY
Image captionMsukumo wa rais Recep Tayyip Erdogan kuwepo kwa rais mwenye mamlaka makuu ilishinda na zaidi ya kura asilimia 51.
Gani jipya ndani ya katiba mpya?
Rasimu inasema kuwa uchaguzi ujao wa rais na bunge utakuwa tarehe 3 Novemba 2019.
Rais atashikilia usukani kwa miaka mitano, na hatapitisha vipindi viwili.
  • Rais ataweza kuchagua maafisa wa juu serikalini wakiwemo mawaziri.
  • Ataweza kuwapa kazi naibu rais mmoja au marais kadhaa.
  • Nafasi ya waziri mkuu ambayo kwa sasa inashikiliwa na Binali Yildirim, itafutwa.
  • Rais atakuwa na nguvu za kuingilia kati mahakama, ambayo Bw Erdogan ameikashifu kwa kuathiriwa na Fethullah Gulen, mhubiri kutoka Pennsylvania anayemlaumu kwa mapinduzi yaliyofeli Julai.
  • Rais ataamua iwapo ataweka hali ya hatari nchini au la.
Maelfu ya watu wameshikwa na takribran watu 100,000 wamefutwa au kuachishwa kazi kwa muda tangu jaribio la mapinduzi Julai mwaka uliopita.Haki miliki ya pichaBURAK KARA/GETTY IMAGES
Image captionMaelfu ya watu wameshikwa na takribran watu 100,000 wamefutwa au kuachishwa kazi kwa muda tangu jaribio la mapinduzi Julai mwaka uliopita.

Serikali ya wakati wa hatari

Waturuki wengi tayari wanahofia utawala wa kimabavu nchini mwao, ambapo maelfu ya watu wameshikwa na takribran watu 100,000 wamefutwa au kuachishwa kazi kwa muda tangu jaribio la mapinduzi Julai mwaka uliopita.
Kampeni zilifanywa wakati wa hali ya hatari baada ya jaribio la mapinduzi kufeli.
Bw Erdogan alichukua usukani kama rais mwaka wa 2014 baada ya kuhudumu kwa zaidi ya muongo mmoja kama waziri mkuu.

MUSIC