Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Tuesday, October 17, 2017

HII KALI NYINGINE,NASSARI KUPELEKA USHAHIDI MWINGINE

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) amewasilisha ushahidi mwingine kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu tuhuma za ununuzi wa madiwani wa Chama hicho.

Madiwani hao nane wa Chadema wamejiuzulu kwa kile walichoeleza kumuunga mkono Rais John Magufuli jambo ambalo Nassari anadai siyo kweli bali walinunuliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya ofisi ya Takukuru Upanga jiji ni humo alisema, " huu ni ushahidi wa tatu na kadri upepelezi ukiwa unaendelea nitaleta mwingine, hii ni kama filamu ya Isidingo."

Nassari alisema alitarajia Rais John Magufuli angewachukulia hatua wateule wake wanaohusishwa katika sakata hilo ili kupisha uchunguzi uweze kufanyika kwa uhuru.

"Tunajiuliza kwa nini Rais hawachukulii hatua DED, DAS au DC wote wa Arumeru kwa kutuhumiwa, watupeleke mahakamani na tungeomba suala hili lichukuliwe kwa uzito wake," alisema Nassari

Naye Mbunge wa Ubungo, Saed Kubunea aliyeongozana na Nassari alisema,"Mimi nimeshiriki hususani kihabari kwani nimewashauri hawa kuutoa kwa umma ili jamii ijue ukweli."

"Tunachojiuliza kwa nini rais yupo kimya, kwa nini mawaziri na viongozi waliotuhumiwa Katika sakata la Almas na Tanzanite aliwasimamisha kwa nini hawa hataki," amehoji Kubenea

Friday, April 21, 2017

Mengine aliyofunguka Nape baada ya kutoka kwenye Uwaziri

Kupitia habari ya Azam Two ya April 20 2017 aliyekuwa waziri wa Habari ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mtama Nape Nnauye amekiri kuwa kuondolewa kwake kwenye nafasi ya uwaziri kuna maswala mengine na hakuna atakaye thubutu kuyaongelea yote yaliyasababisha kutokea kwa jambo hilo.
Nape amezungumza na mwandishi wa habari wa Azam two na kusema kuondolewa kwake katika wadhifa huo kulishatabiliwa kutokana na maswala aliyokuwa akiyasimamia na misingi ambayo anayoiamini na hivyo asingependa kwenda kinyume kwa hicho anachokiamini na hakushtushwa na maaamuzi yaliyochukuliwa na mteule wake.

Monday, January 4, 2016

CCM yambana Lowassa

Aliyekuwa mgombea urais wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimemtaka aliyekuwa mgombea urais wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, kutaja majina ya wafanyabishara aliodai wanaotozwa kodi kubwa na serikali kwa sababu walivisaidia vyama vya upinzani wakati wa kampeni.
 
Chama hicho kimesema endapo Lowassa asipofanya hivyo, lengo lake litakuwa ni kutaka kuigombanisha serikali iliyoko madarakani na wafanyabiashara wakubwa ambao ndiyo walipaji kodi wa nchi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM (Taifa), Abdallah Bulembo, alisema endapo Lowassa asipowataja wafanyabishara hao atakuwa amesababisha wasiwasi mkubwa kwa wafanyabishara ambao waliwasaidia kipindi cha uchaguzi mkuu.
Aidha, Bulembo alisema madai hayo ya Lowassa yanaweza kusababisha wafanyabiasha hao ambao ndiyo wanaolipa kodi kuingiwa na wasiwasi wa kutozwa kodi kubwa na serikali.
 
Alisema masuala ya uchaguzi kwa sasa yameshamalizika hivyo Lowassa anapaswa kutaja majina ya wafanyabishara hao ambao anadai wanatozwa kodi kubwa kwa kukomolewa kwa sababu walivisaidia vyama vya upinzani.
 
“Maneno aliyayatoa Lowassa dhidi ya serikali yanaweza kudhoofisha kasi ya serikali ya Rais Dk. Magufuli ya kukusanya kodi. Kazi ya serikali ni kukusanya kodi, hivyo aiache ikusanye kodi kwa maendeleo ya taifa,” alisema na kuongeza:
 
“Lowassa ni mtu mkubwa sana hapa nchini, akisema neno linaweza kuleta madhara makubwa, hivyo anapaswa kutaja majina ya wafanyabishara hao kama wapo hata mia moja, ili watu wahoji kuwa awali walikuwa wanalipa kodi shilingi ngapi na hivi sasa wanatozwa shilingi ngapi.” 
 
Bulembo aliongeza kuwa, kwa sasa serikali ya Rais Magufuli imeongeza makusanyo ya kodi kutoka Sh. bilioni 800 hadi kufikia Sh. trilioni 1.3, hivyo anapaswa kuungwa mkono badala ya kutoa kauli zinazoweza kumkwamisha.
SHULE ZA CCM
 
Aidha, Bulembo alisema shule 26 za Jumuiya ya Wazazi ya CCM, zilifanyiwa ukaguzi mwaka jana na kubainika 15 zina ubadhirifu wa fedha.
 
Alisema kutokana na hali hiyo, wahusika wote waliobainika katika kashfa hiyo watafikishwa katika vyombo vya sheria.
 
“Naomba wenyeviti wenzangu wa mikoa waache ukaguzi ufanyike, hatua zinazochukuliwa sasa ziendelee kuchukuliwa wala wasiogope na kutotoa ushirikiano ili wasije wakaingia katika migogoro,” alisema Bulembo.
 
Alisema hadi sasa kuna shule nne za jumuiya hiyo ambazo zimepelekwa mahakamani kutokana na ubadhirifu huo, hivyo viongozi walioko mikoani waone kinachotendeka kwa sasa ni halali na hakuna atakayeonewa.
 
Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Alisema miaka mitatu iliyopita wakati uongozi wake ukiingia madarakani, mapato kwa mwaka kutokana na miradi yake yote yalikuwa ni Sh. milioni 50, lakini kwa mwaka huu yameongeza na kuwa Sh. bilioni 1.6 kwa mwaka.
 
ADA ELEKEZI
Kuhusu ada elekezi, Bulembo alisema Jumuiya ya Wazazi ya CCM itaendelea kutoza ada kwa shule zake kwa kiwango cha zamani bila ya kufuata bei elekezi iliyotolewa na serikali.
 
Alisema CCM itakutana na serikali kuzungumzia suala hilo la ada elekezi kwa kuwa utekelezaji wake ni mgumu.
 
AMJIBU MAKONGORO MAKATIBU WAKUU
Bulembo alisema Rais Magufuli ameunda baraza la mawaziri lenye wizara 19 ikiwa ni idadi ndogo kuliko serikali iliyopita iliyokuwa na baraza la mawaziri 31.
 
Alisema kauli iliyotolewa na aliyekuwa Naibu wa Wizara ya Kazi na Ajira ambaye kwa sasa amehamia Chadema, Makongoro Mahanga, kuwa serikali hiyo ni kubwa kuliko iliyopita haina mashiko , kwani Rais Magufuli ameteua baraza la Mawaziri kwa kuzingatia ufanisi na utendaji makini.
 
Alisema Rais Magufuli ametimiza siku 60 tangu aapishwe kuwa Rais wa tano wa Tanzania, hivyo anapaswa kupewa muda wa kiutendaji zaidi.
Alisema kauli za vyama vya upinzani kudai kuwa Rais Magufuli anatekeleza ilani ya upinzani haina ukweli wowote, kwani mengi yamo ndani ya Ilani ya CCM likiwamo la kupambana na mafisadi na hata wakati wa kampeni zake alikuwa akieleza wazi.
 
Hivi karibuni vyombo vya habari vilimkariri Lowassa zungumza akiwa mkoani Tanga akidai serikali kuwatoza kodi kubwa wafanyabiashara waliokisaidia Chadema wakati wa kampeni na kuitaka CCM kuacha vitendo hivyo.
 
Lowassa alikaririwa akidai kuwa, imezuka tabia ya kuwanyanyasa wafanyabiashara waliounga mkono Chadema na kuitaka serikali ya Rais Dk. Magufuli iache mara moja.
 
CHADEMA WAZUNGUMZA
Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene, alipotafutwa kulizungumzia suala hilo,  alisema suala la kutaja majina siyo kazi yao.
 
Alisema Lowassa alichokieleza ni kuwa kuna mkakati wa serikali kushughulikia wafanyabiashara waliokuwa wanamuunga mkono wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
 
Alisema Chadema siyo kazi yake kutaja majina ya watu, bali inahitaji kuona Watanzania wote wanatendewa sawa bila ya ubaguzi wowote.
 
CHANZO: NIPASHE

Monday, November 9, 2015

LOWASA AHOJI MASWALI MAGUM KWA MH.MAGUFULI

Edward Lowassa.

Aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
 
Edward Lowassa, amehoji maswali matatu kwa Rais Dk. John Magufuli.Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Lowassa amemtaka Rais Magufuli baada ya kusema hakuna mtoto atakayelipa ada kuanzia Januari, mwakani, atamke mustakabali wa wanafunzi walioko shuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.
 
Lowassa amesema kwa upande wake ahadi ya elimu bure aliyokuwa akiinadi wakati wa kampeni, ilikuwa ni kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu na kwamba hata wale walioko mashuleni, wangeguswa na hatua hiyo.
 
“Niliahidi watoto wote walioko na watakaoanza shule kuanzia kindergarten (shule ya awali) hadi chuo kikuu, serikali yetu ingegharimia. Na nilitangaza kufuta michango yote shuleni ili kumpunguzia mzigo mwananchi,” alisisitiza Lowassa ambaye amekataa kuyatambua matokeo ya ushindi wa Dk. Magufuli akidai kuwa yeye ndiye aliyeshinda kwa asilimia 62 ya kura zote zilizopigwa.
 
Kuhusu suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, Lowassa amesema yeye alishaweka wazi kuwa elimu ingekuwa bure hadi chuo kikuu.
 
“Vijana hawa wanahangaika na mikopo na nasikia ni asilimia 17 tu kati ya wanafunzi 70,000 ndiyo waliopata mikopo. Sera ya Chadema na Ukawa kwa ujumla, ni kufuta kabisa shida hizi kwa serikali kufadhili elimu yao,” alifafanua Lowassa katika taarifa yake hiyo. Kwa msingi huo, Ukawa kupitia kwa aliyekuwa mgombea wao wa urais, Lowassa, umewataka wananchi kutofautisha ahadi ya elimu bure iliyotolewa na Rais Magufuli na ile iliyotolewa na Ukawa.
 
Lowassa alisema Magufuli ametoa maelekezo kwa watendaji wa serikali kuweka mikakati ya kutekeleza ahadi yake kuanzia Januari, mwakani kwamba hakuna mtoto atakayelipa ada.
 
Hata hivyo, amesema hajaeleza waziwazi hatma ya wanafunzi walioko mashuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.
 
CHANZO: NIPASHE

Saturday, October 10, 2015

LOWASSA, KINGUNGE 'MOTO' ARUSHA


MKUTANO wa mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA, Edward Lowassa, jana uliweka historia mkoani Arusha baada ya wafanyabiashara kuamua kusitisha huduma zao na kwenda kumsikiliza mgombea huyo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Viwanja vya Sinoni.

Uwanja huo ulianza kujaa asubuhi ambapo kivutio kikubwa kilikuwa kwa mwanasiasa mkongwe ambaye hivi karibuni alitangaza kujiondoa CCM, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.

Akihutubia mkutano huo, Mzee Kingunge alisema ipo haja ya wananchikumchagua Lowassa awe Rais wa Awamu ya Tano ili aweze kuwaletea mabadiliko wanayoyahitaji.

Alisema Lowassa ana uwezo mkubwa wa kubadili maisha ya wananchina Tanzania kwa ujumla tofauti na CCM ambayo viongozi, wagombeawake hutumia muda mwingi majukwaani kuwashambulia wapinzani.

"Viongozi wa CCM wamesahau kauli ya hayati Mwalimu Nyerere aliposema watu wakikosa mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta njeya chama hicho; hivyo mchagueni Lowassa anatosha," alisema.

Aliongeza kuwa, viongozi wa CCM badala ya kunadi sera za chama chao, wanatumia majukwaa kutukana.

"Baada ya siku nne kuanzia leo, nitatoa siri nzito za CCM, nawaomba Watanzania msidanganyike na kitu chochote, CCM si chama bora, angalieni sera za Lowassa," alisema Mzee Kingunge.

Naye Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, James Mbatia, alisema watu  wanaoambiwa mgombea urais wa CCM, Dkt. John Magufuli ndiyeanayefaa kuwa rais wanadanganywa.

Alisema mgombea huyo hana sifa za kuwa rais kama inavyodaiwa kwani utendaji kazi wake hauwezi kufanana na ule wa Lowassa.
Lowassa akerwa na umaskini.

Kwa upande wake, Lowassa alisema anakerwa na umaskini mkubwa walionao Watanzania; hivyo aliwaomba wamwamini kwa kumpigia kura za kutosha ili Serikali ambayo ataiunda iweze kukata kiu yao.

"Mlo mmoja wanaokula Watanzania utabaki kuwa historia, nataka kila Mtanzania ale milo mitatu kwa siku...nashangazwa na CCM inaposema itaboresha maisha ya Watanzania wakati uwezo huo hawana.

"Watanzania wengi wanateseka kutokana na ugumu wa maisha, hatakupata mlo mmoja ni shida...nauchukia umaskini, nikiingia Ikulu nitahakikisha sekta zote zinapiga hatua ya maendeleo," alisema.

Aliongeza kuwa, inashangaza kuona baadhi ya watoto wanakosa elimu,  nchi ina rasilimali za kutosha kama madini, hifadhi za wanyama na gesi ambazo zinatosha kufuta umaskini.

"Mtoto wa Serikali ya Lowassa lazima asome hadi Chuo Kikuu bure, hikini kipaumbele changu, nipeni kura niwatumikie na kumaliza kero zenu mbalimbali zilizoshindwa kupatiwa ufumbuzi," alisema.

MAGUFULI AMLIPUA MBATIA, AMPIGIA DEBE MREMA


MGOMBEA urais wa CCM, Dkt. John Magufuli, amewataka wakazi wa Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro, kutompigia kura mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Alisema kama hawataki kumpigia kura mgombea ubunge wa CCM, Bw. Innocent Shirima, basi wanaweza kumchagua Mwenyekiti wa TLP anayegombea ubunge jimboni humo, Augustino Mrema.

Dkt. Magufuli aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Himo akisema Mbatia amekuwa akimnyima amani Mrema mbali ya kuondoka NCCR-Mageuzi, lakini bado amekuwa akimfuata jimboni; hivyo wamnyime kura kwani hafai kuwaongoza.

"Kama hamtaki kumchagua mgombea ubunge wa CCM, mchagueni Mrema ambaye mara nyingi amekuwa akiwatetea bungeni...simaanishimsimchague Shirima, huyu ndiye ninayemhitaji ili niweze kumtumia katika harakati za maendeleo ya jimbo hili," alisema.

Aliongeza kuwa, Mbatia ameshindwa kukijenga chama chake badala yake amekuwa akijivika vyeo ndani ya UKAWA, hivi sasa amekuwa msemaji wa CHADEMA na kukiacha chama chake.

Aliufananisha UKAWA na magari manne ambayo yote ni mabomu yanayoshindana na gari jipya CCM na kuwataka wananchi kutambuakuwa, yeye ndiye Rais wa Awamu ya Tano, hivyo Oktoba 25, mwaka huu, wasihangaike kuwapigia kura wapinzani.

Mrema na Dkt. Magufuli uso kwa uso
Katika hatua nyingine, Dkt. Magufuli baada ya kumaliza mkutano Jimbo la Vunjo, akiwa njiani kwenda Wilaya ya Mwanga, msafara wake ulisimamishwa njiani na Mrema ambaye aliwasihi wakazi wa Himo wamchague Dkt. Magufuli kuwa rais wao.

"Dkt. Magufuli ni mchapakazi na ndiye rais wetu, hakikisheni Oktoba 25, mwaka huu, mnampigia kura nyingi...amefanya mengi ndani ya CCM kwani amejenga barabara nyingi katika wilaya hii," alisema.
Jimbo la Rombo
Awali, Dkt. Magufuli akiwa wilayaji Rombo, aliwataka wakazi wa Tarakea kumtafutia kazi ya kufanya mgombea ubunge wa CHADEMA, Joseph Selasini kwani hatoshi kuwa mbunge wao, ameshindwa kazi.

Alisema Selasini hafai kuwa mbunge kwani miaka yote aliyokaa bungeni alikuwa akitoka nje wakati Bunge likijadili matatizo ya Watanzania.

Dkt. Magufuli aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Tarakea Mpakani akiwataka wananchi wafanye mabadiliko ya mbungena kumchagua wa CCM badala ya kuendelea kumsikiliza Freeman Mbowe ambaye naye ameshindwa kuwasaidia wananchi.

Wilaya ya Mwanga
Akiwa katika Wilaya ya Mwanga, Dkt. Magufuli alisisitiza kuwa yeye ni tingatinga ambalo kazi yake ni kufanya kazi; hivyo atahakikisha muda wote anawatumikia Watanzania ili aweze kuleta mabadiliko nchini.

"Nawaomba mnichagulie wabunge na madiwani wote wa CCM ili niweze kuwatumia kuharakisha maendeleo yenu...ukimpenda Magufuli lazima upende na funguo, mimi ndiye ninayetosha kuwa rais," alisema.

Thursday, October 8, 2015

JK aongoza maelfu kumuaga Mchungaji Mtikila


Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal akiongoza mamia ya wananchi kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha DP, Christopher Mtikila wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam jana. (Picha na Yusuf Badi).

                                                            

RAIS Jakaya Kikwete ameongoza mamia ya waombolezaji pamoja na viongozi wa kitaifa, katika kumuaga Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila aliyekufa kwa ajali hivi karibuni mkoani Pwani.
Katika shughuli hiyo, viongozi wengi waliohudhuria walimuelezea Mtikila kuwa ni mwanaharakati wa mageuzi, aliyeipigania Tanganyika mpaka kifo chake, lakini pia alisimamia na kuheshimu taratibu za kisheria na kutaka mabadiliko bila uoga.
Rais Kikwete alifika katika shughuli hiyo ya kumuaga Mtikila iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, akiambatana na Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.
Viongozi wengine waliohudhuria shughuli hiyo ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, Msajili wa zamani wa vyama hivyo, John Tendwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.
Pia walikuwepo Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Peter Mziray ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha PPT-Maendeleo, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari na Naibu Katibu Mkuu wa TLP, Dotnata Rwechungura.
Akizungumza katika shughuli hiyo ya kumuaga Mtikila ambaye jeneza lake lilifunikwa kwa bendera ya Tanganyika, Msajili wa Vyama vya Siasa, Mutungi aliwataka watanzania kumuenzi mchungaji huyo kwa matendo yake ya kuchukia vurugu na badala yake aliamini zaidi katika sheria.
“Mchungaji Mtikila atakumbukwa kwa misimamo yake mikali. Alipenda kusimamia kile anachokiamini. Lakini kubwa zaidi alitoa mchango katika nyanja ya Sheria, kwa sasa huwezi kuzungumzia masuala ya sheria hususani haki za binadamu bila kumtaja Mtikila,” alisema Mutungi.
Alisema kupitia sekta ya Sheria, mwanaharakati huyo alifanikisha mabadiliko kadhaa, ikiwemo kuingizwa kwenye Katiba kwa kifungu kinachoruhusu mgombea binafsi, lakini pia alifanikisha kubadilishwa kwa kifungu kinachohusu maandamano.
“Huyu alikuwa ni mpambanaji, alifungua kesi nyingi kwa kuwa aliamini katika kufuata sheria na si kuandamana au kufanya vurugu. Naomba tumuenzi kwa kutopenda kushinikiza fujo na maandamano, vyombo vya sheria vipo kama kuna tatizo tuvitumie kutafuta haki,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Dk Bilal alimtaja Mchungaji Mtikila kuwa alikuwa ni mtu jasiri, aliyeshirikiana na wenzake bila kujali tofauti za mitazamo waliyonayo. “Mimi nilimfahamu Mtikila kupitia uanaharakati wake wa kutaka mabadiliko, ni kweli alikuwa anataka sana kuirejesha Tanganyika, lakini pamoja na tofauti za fikra zetu, alikuwa anakuja hadi ofisini kwangu kipindi kile nilikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia na tulikuwa tunazungumza sana,” alisema.
Aliwataka watanzania kuiga mfano wa matendo ya Mtikila, kwani kwa sasa nchi inataka watu kama hao wenye mawazo mapya na hawaogopi kuyatoa na kuyatetea bila kudharau mawazo na fikra za wengine.
Maalim Seif, kwa upande wake, alisema alifahamiana na Mtikila kupitia harakati zake za kisiasa na kubainisha kuwa ni mtu anayejiamini, asiye uoga na mwenye kuajimini na kusimamia kile anachokiamini.
Mziray alisema anaipongeza Serikali kwa kitendo chake cha kushirikiana na familia ya Mtikila kwa hali na mali, bila kujadili kuwa ni mwanaharakati wa mabadiliko, jambo alilosisitiza kuwa hiyo ndio Tanzania inayotakiwa kwa sasa.
Makamu Mwenyekiti wa DP, Peter Mwagila alibainisha kuwa chama hicho kimepata pigo na pengo kubwa kwa kuondokewa na mwenyekiti wao, ambaye pia pamoja na kuwa muasisi wa chama hicho, ni mwanaharakati wa mageuzi aliyepigania nchi yake ya Tanganyika.
“Mtikila ndoto zake zilikuwa ni kurejeshwa kwa Tanganyika ambayo iliondolewa kwenye ramani ya dunia tangu mwaka 1962, alitaka kuwepo na Rais wa Tanganyika, Katiba, wabunge na mamlaka zote za nchi ya Tanganyika. Lakini pia alipinga rushwa, ufisaidi na kuwachukia viongozi wanaojilimbikizia mali,” alisema.
Alisema chama hicho kitahakikisha kinaendeleza na kusimamia harakati zote zilizoanzishwa na Mtikila ikiwemo kuidai Tanganyika. Msemaji wa familia ya mchungaji huyo, Peter Mayani, wakati akisoma wasifu wa Mtikila, alisema mwanaharakati huyo alibobea katika fani za sheria, uchumi na masoko na aliwahi kuajiriwa Mahakama Kuu na Shirika la Ndege la Afrika Mashariki, ambalo alilitumia kutoroshea wanaharakati wa chama cha Frelimo.
Alisema Mtikila aliokoka rasmi mwaka 1983 na kuanzisha Kanisa la Pentekoste la Full Salvation na mwaka 1990 alianza harakati za ukombozi, zilizoshinikiza kuanzishwa kwa vyama vingi mwaka 1992. Pia alianzisha chama cha DP, ambacho kilichelewa kupata usajili wake hadi mwaka 2000.
Mtikila baada ya kuagwa alisafirishwa kwenda kijijini kwao Milo, wilayani Ludewa mkoani Njombe ambako anatarajiwa kuzikwa leo. Marehemu ameacha mjane Georgia Mtikila. Askofu wa Kanisa la Ufunuo, Nabii Paul Bendera, aliwataka watanzania kutambua kuwa wote ni wageni duniani na kwamba kila mtu bila kujali ni nani duniani na ana cheo gani iko siku yake atakufa.
“Kwa sasa hali imekuwa ngumu na mbaya nawaomba ndugu zangu tuwe makini, lakini kubwa zaidi kila mtu amheshimu maisha ya mwenzake tuweke upendo na amani mbele na hii iwe ndio kipaumbele chetu. Naomba Serikali nayo iongeze juhudi za kuwalinda wananchi wake,” alisisitiza.
Mchungaji Daudi Mwaijojele, alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania kuacha uchafu na kumrejea Mungu, ili kutengeneza maisha yao ya baadaye pindi watakapokufa. “Nawaomba acheni uchangudua, ufisadi na michepuko tena hiyo michepuko ndio inaleta magonjwa kama vile Ukimwi majumbwani na kusambaratisha familia,” alisema.
Mtikila alikufa kwa ajali ya gari aina ya Toyota Corolla, lenye namba za usajili T 189 AGM maeneo ya Msolwa wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani. Alikuwa akitokea Njombe kwenda Dar es Salaam.

Magufuli ashambulia jimboni kwa Mbowe.


Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli.

  Apokelewa kwa mabango yanayoelezea kero za maji, barabara, elimu na afya.
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, ametikisa katika Jimbo la Hai na kumshambulia Mbunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema aliyemaliza muda wake,  Freeman Mbowe  kwamba ni Mbunge mtalii anayeshinda akizurura Ulaya, huku akishindwa kutatua kero za wapiga kura wake.
 
Akihutubia jimboni humo katika siku yake ya kwanza ya kampeni mkoani Kilimanjaro jana, Dk. Magufuli (pichani) aliwaambia wananchi wa jimbo hilo kwamba, walifanya biashara ya hasara kumchagua Mbowe kuwa Mbunge wao kwani hajali maslahi ya wananchi wake.
 
Awali mgombea huyo wa CCM alipokelewa na umati wa jimbo hilo kwa mabango yenye ujumbe mbalimbali yanayoelezea kero za maji, barabara, elimu na afya, ambayo aliagiza yachukuliwe na msafara wake ili atakapoingia Ikulu azifanyie kazi kero hizo.
 
Dk. Magufuli alisema wananchi wa Jimbo la Hai wameteseka kwa muda mrefu kwa kuwa na Mbunge ambaye kazi yake imekuwa kuzunguka jijini Dar es Salaam na mataifa ya Ulaya na Marekani, huku jimbo likikabiliwa na matatizo ya kijamii kama maji, elimu na ukosefu wa huduma za afya.
 
“Ingawa nampenda Mbowe, lakini wananchi wa jimbo hili wanapaswa kufanya mabadiliko kwa kumtosa Mbunge huyo  abaki na nafasi yake ya uenyekiti wa Chadema ili akaimarishe chama hicho na wamchague mbunge wa CCM ambaye atawasaidia,” alisema.
 
Kwa mujibu wa Dk. Magufuli, Mbowe hawezi kushughulikia masuala ya maendeleo kwa kuwa anakabiliwa na majukumu mengi ya biashara na uenyekiti wa Taifa wa Chadema.
 
“Mbowe ana nipenda na huwa ana nisifia hadharani kwamba mimi ni mchapakazi na mimi pia nampenda sana lakini kwenye masuala ya maendeleo ya Watanzania sitaweka urafiki achaneni naye na mumchague Dunstan Mallya wa CCM awafanyie kazi watu wa Hai.” alisema mgombea huyo wa CCM.
 
Alisema hata Halmashauri ya Wilaya ya Hai ambayo inaongozwa na Chadema imeshindwa kuondoa kero za wananchi na kuongeza kuwa ingawa wilaya hiyo ni ya zamani imebaki nyuma kwa miaka mingi kulinganisha na wilaya mpya.
 
SIHA
Akiwahutubia wananchi wa Siha, mkoani hapa jana, Dk. Magufuli alisema ameshajihakikishia ushindi wa kishindo na kudai wapinzani wanamsindikiza na kuwataka wananchi wa jimbo hilo wamchague Agrey Mwanri kwa mara nyingine awe Mbunge wao kutokana na kazi nzuri aliyowafanyia.
 
DK. NCHIMBI
Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), Dk. Emmanuel Nchimbi, aliibukia kwenye kampeni za Dk. Magufuli wilayani Siha na baadaye Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro jana na kumrushia makombora mgombea urais  wa Ukawa, Edward Lowassa.
 
Dk. Nchimbi ambaye alikuwa swahiba mkubwa wa Lowassa kwenye harakati za kuwania kuteuliwa na CCM kuwania urais, alidai Lowassa ni dhaifu na hawezi kuiongoza Tanzania.
 
Nchimbi alisema Watanzania wanahitaji  Rais aina ya Magufuli ambaye atawaendesha mchakamchaka wa maendeleo na si wagombea wengine ambao historia zao zinaonyesha walishindwa kwenye nafasi za juu walizowahi kushika.
 
CHANZO: NIPASHE

MUSIC