Monday, May 8, 2017

Wizi wa Punda tishio Kenya, ngozi yake ndio kitu pekee Wezi wanachukua

CITIZEN TV ya Kenya imeripoti taarifa ya wizi wa punda uliokithiri huko Turkana kiasi kwamba hata Wakazi wenyewe wamejawa na hofu na kisa kikiwa ni kuuzwa kwa ngozi ya punda hao.
Biashara ya kuuzwa ngozi ya punda inadaiwa kuwa imeletwa na Wachina na kufanya ngozi ya mnyama huyo kupanda thamani hadi shilingi za Kenya 10,000 ambazo ni zaidi ya shilingi laki mbili za Tanzania huku Punda mwenyewe akiuzwa Ksh 5000 (laki moja na elfu nane ya Tanzania).
Wanasema baada ya Wachina kuinunua ngozi hiyo husafirishwa na kwenda kutumika kwenye kutengeneza dawa inayotibu magonjwa mbalimbali kwenye mwili wa binadamu.
...>>>”Unaweza nunua punda kwa elfu 5 au sita na ukauza ngozi kwa Elfu 10 hali hiyo ikaleta thamani ya Punda na ndiomaana wezi wanaiba Punda na kumchuna ngozi ili aje auze ngozi peke yake” – Joseph Losuru 
“Tuliona kwenye media za Nigeria kuwa Punda wameisha lakina na hapa kwetu pia Punda wameanza kuisha” – Lokwale Anton Mfugaji

Monday, May 1, 2017

Nape Nnauye amkumbuka Mwalimu Nyerere

Mbunge wa jimbo la Mtama, Mh Nape Nnauye amemkumbuka marehemu baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuamua kutumia maneno yake katika kufikisha ujumbe wake kwa wananchi kupitia ukurasa wake wa twitter 
Mhe Nape Nnauye alikuwa akitoa ujumbe kuwa maana ya ubinadamu na heshima ya binadamu ni kutokaa kimya pale jambo la uovu linapokuwa likitokea, akiwataka wananchi kutokaa kimya wanapoona kuna jambo la uovu linatendeka.
Ili kufikisha ujumbe huo vizuri Mhe. Nape Nnauye ilibidi atumie clip ya video ya marehemu baba wa taifa, Julius Kambarage Nyerere wakati akihotubia kwa mara ya mwisho katika Mkutano Mkuu. Ambapo mwalimu alisema maneno haya kwa lugha ya kiingerza  
"Hotuba yangu ya mwisho kwenye huu mkutano mkuu, nimeelezea matukio na mienendo na mahitaji kwa namna ambavyo sisi Watanzania tuonavyo, kukaa kimya pale tuonapo hatari, kutulia tu pale tuonapo sera hatari ambazo ziko kinyume na kulinda amani na haki, kufanya hivyo itakuwa tunaachia uhuru wetu na utu wetu kamwe hatutafanya hivyo" Mwalimu Nyerere 
Baada ya kuweka video hiyo ya Mwalimu Nyerere Nape Nnauye naye aliweka ujumbe wake ambao ulisomeka hivi 
"Heshima ya binadamu na maana ya kweli ya ubinadamu ni kutokaa kimya pale uovu unapotendeka" aliandika Nape Nnauye   

Rais Magufuli atoa onyo kwa makampuni ya simu nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametahadharisha kuwa, wapo mbioni kuhakikisha mapato ya serikali yanadhibitiwa zaidi ili taifa liweze kujitegemea kikamilifu, huku akionya makampuni ya simu nchini.
Rais Magufuli ameyasema hayo Ijumaa hii, mjini Dodoma wakati akikabidhiwa taarifa ya vyeti feki. Rais ameyaonya makampuni hayo, akisema, dawa ya makampuni hayo bado inatengenezwa.
“Bado kuna maeneo mengi ambayo tunaibiwa fedha. Kwenye haya makampuni ya simu haya, yanafanya transactions nyingi lakini hela haziingii serikalini, dawa yao tunaitengeneza baada ya muda mfupi kidogo itakamilika,” alisema Rais Magufuli huku akishangiliwa.

Sunday, April 30, 2017

MBAO FC YAIVUMUA YANGA

Baada ya Jumamosi ya April 29 Simba kucheza mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Azam FC na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Mohamed Ibrahim dakika ya 48, Yanga leo walishuka dimba kucheza nusu fainali dhidi ya Mbao FC.
Yanga waliingia katika uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Mbao FC katika mchezo huo wa nusu fainali, kabla ya mchezo kumalizika Yanga ndio alikuwa Bingwa mtetezi wa michuano hiyo, kwa bahati mbaya Yanga amevuliwa Ubingwa kwa kufungwa goli 1-0 lililopatikana kwa beki wake Andrew Vincent kujifunga dakika ya 27.
Ushindi wa Mbao FC ambao wanaingia fainali hiyo kwa mara ya kwanza ikiwa ni msimu wao wa kwanza toka wapande kucheza Ligi Kuu, unaifanya sasa kukutana na Simba katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo ya Kombe la FA (ASFC) katika tarehe ambayo itatajwa na TFF.

Friday, April 28, 2017

Zlatan Ibrahimovic amekataa kulipwa mshahara na Man United

Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic amerudi kwenye headlines baada ya maamuzi yake kuandikwa na vyombo vya habari, Zlatan ameripotiwa na mtandao wa dreamteamfc.com kuwa amekataa kulipwa mshahara na Man United.
Zlatan Ibrahimovic atakuwa nje ya uwanja katika kipindi cha miezi 9 baada ya kuumia goti lake la kulia wakati wa mchezo wa marudiano wa  Europa League dhidi ya Anderltch ya UbelgijiZlatan anayelipwa mshahara wa pound 250000 kwa wiki alijiunga na Man United kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Baada ya kujulikana kuwa Zlatan atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 9 Man United walikuwa wapo tayari kuendelea kumlipa mshahara kama kawaida katika kipindi chote cha majeruhi lakini Zlatan amekataa, Zlatan anatarajiwa kurudi uwanja kuanzia mwezi Janury 2018.

Bashe aishukia serikali ya Kenya

Mbunge wa Nzega mjini, Hussein Bashe amesikitishwa na Serikali ya Kenya kuweka zuio la kuingiza mitungi ya gesi inayotoka Tanzania na kusema ni vizuri nchi hiyo ikaheshimu mikataba ya ‘East African Community (EAC) .
Mbunge huyo ameandika hayo kupitia ukurasa wake Twitter hivi:
Quality ,Dar port and Cost ya Gesi inayotoka Tz ndo competitive edge ya Ma kampuni ya Tz dhidi ya Yale ya kenya uamuzi huu si sawa.
Serekali ya Kenya imezuia Gesi za matumizi ya nyumbani zinazotoka Tz kuingia Kenya ni vizuri Kenya ikaheshimu EAC treaty “Common mkt”
Bashe amesema hayo baada ya serikali ya Kenya, kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Andrew Kamau kupiga marufuku uagizaji wa gesi ya kupikia kutoka Tanzania kupitia mipaka ya nchi hiyo.

Meli ya kijasusi ya Urusi yazama Uturuki

Meli ya Liman ikipitia mlango wa bahari wa Bosphorus mwezi OktobaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli ya Liman ikipitia mlango wa bahari wa Bosphorus mwezi Oktoba
Meli ya kijasusi ya Urusi imezama baharini katika pwani ya Uturuki baada ya kugongana na meli ya kubeba mizigo, maafisa wa uchukuzi wa baharini wa Uturuki wamesema.
Wote waliokuwa kwenye meli hiyo wameokolewa.
Urusi awali ilikuwa imethibitisha kwamba meli ya Liman, ambayo ni sehemu ya kundi la meli za taifa hilo katika Bahari Nyeusi ilikuwa imepatwa na hitilafu na kwamba juhudi za kuizuia kuzama zilikuwa zinaendelea.
Chanzo cha kugongana kwa meli hizo hakijabainika lakini kulikuwa na ukungu mwingi eneo hilo.
Meli hiyo ya kijasusi iligonga meli yenye bendera ya Togo ambayo ilikuwa ikisafirisha mizigo, vyombo vya habari Uturuki vinasema.
Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildirim amezungumza na mwenzake wa Urusi Dmitry Medvedev, na kumueleza masikitiko na huzuni yake kutokana na ajali hiyo, duru katika afisi ya waziri mkuu huyo wa Uturuki zimenukuliwa na shirika la habari la Reuters.
Kundi la Meli za Urusi Bahari Nyeusi (BSF) hupitia mlango wa bahari wa Bosphorus Strait kuelekea bahari ya Mediterranean, ambapo hushiriki katika harakati za kijeshi Syria.
Meli hiyo ya Urusi ilikuwa na watu 78 ambao waliokolewa wote.
Ramani
Meli hiyo iligongana na meli ya Youzarsif H takriban 29km kutoka mji wa Kilyos kaskazini mwa mji wa Istanbul.
Haijabainika iwapo meli hiyo ilikuwa inaelekea mlango wa bahari wa Bosphorus wakati huo.

Man City na Man United HAKUNA MBABE

eplHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWachezaji wa City na United
Mchezo wa dabi ya jiji la Manchester kati ya Mashetani wekundu wa Man United na Man City umemalizika kwa sare ya bila kufunga mchezo huo ulipigwa katika dimba la Etihad.
Kutoshana nguvu kwa timu hizi kunafanya vita ya kuwania nafasi nne za juu kuendelea kuwa kali City wako nafasi ya nne kwa alama 65 alama moja mbele ya United walioko nafasi ya tano kwa alaam 64.
Man city wakiwa wenyeji wa mchezo huo waliutawala mchezo kwa asilimia kubwa na umiliki wa mpira ukiwa ni asilimia 69 kwa 31.
United walibaki pungufu katika dakika ya 84 baada ya kiungo wake Marouane Fellaini kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu, baada ya kumpiga kichwa Sergio Aguero.Huu ulikua ni mchezo wa 24 kwa Man united wakicheza bila kupoteza msimu huu

Venezuela kujiondoa kwenye umoja wa OAS

Nchi ya Venezuela imetangaza kujiondoa katika shirika la umoja wa mataifa ya Marekani Kusini (OAS ) kwa madai kuwa, nchi zilizopo ndani ya jumuiya hiyo zinaingilia masuala ya ndani ya nchi yao.
Akiongea na kituo cha runinga cha taifa (VTV), Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Delcy Rodriguez amesema, “Katika OAS, tulitangaza kwamba hatua hizi za usumbufu, zimeegemea upande mmoja, haramu.Tutachukua hatua za haraka za kuandaa barua kwa OAS na kuelezea ni ya kujiondoa kwa Venezuela kwenye huu umoja.”
“Kesho, kama alivyotaka Rais Nicolas Maduro, tutawasilisha barua ya kujiondoa katika umoja wa OAS na tutaanza hatua hizo ambazo zitachukua miezi 24,” ameongeza.
Watu wapatao 30 wamefariki dunia katika maandamano yanayoendelea nchini humo kwa takribani wiki ya tatu sasa,wakimtaka rais Nicolas Maduro kujiuzulu kutokana kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo jambo lililosababisha upungufu mkubwa wa chakula.

US: Mfumo wa kujilinda ''utamuamsha'' rais wa K. Kaskazini

Upelekaji wa mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini ulipingwa na waandamanajiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionUpelekaji wa mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini ulipingwa na waandamanaji
Mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa Marekani unaowekwa nchini Korea Kusini utaanza kufanya kazi katika siku chache zijazo, jeshi la Marekani limesema.
Mfumo huo wa Thaad umetengezwa kuilinda Korea Kusini na majeshi ya Marekani yaliopiga kambi nchini humo dhidi ya vitisho vya Korea Kaskazini.
Vifaa vya mfumo huo vilipelekwa katika taifa hilo siku ya Jumatano, Admirali Harry Harris ambaye ni ni kamanda wa eneo la Pacific alisema kuwa Thaada itaanza kufanya kazi katika siku chache zijazo ili kuiinda Korea Kusini dhidi ya vitisho vya jirani yake Korea kaskazini.

Wanafunzi wanaopata ujauzito waendelee kusoma – Waziri Mwalimu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa mashuleni waendelee na masomo yao, ili kufikia malengo walioyanayo nchini.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa masuala ya kijinsia ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
“Tunapokataza watoto wa kike wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa mashuleni, tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao kwa wakati waliotarajia,”alisema Waziri Ummy.
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha DUCE, Profesa William Anangisye amesema lengo la mkutano huo ni kuleta chachu ya kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kupata wanasayansi wanawake nchini.

Ajuza aliyekataliwa na benki kwa kuwa mzee sana Mexico

María Félix Nava, ana miaka 116Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaría Félix Nava ni miongoni mwa binadamu wazee zaidi kwa sasa duniani
Benki moja nchini Mexico hatimaye imesema itamfungulia akaunti ya benki mwanamke wa umri wa miaka 116 ambaye awali alikuwa amekataliwa kwa sababu ya kuwa mzee sana.
Citibanamex ilikuwa imelaumu hitilafu kwenye mfumo wake wa benki ambayo ilizuia maafisa wake kumfungulia akaunti.
Hatua hiyo ya awali ilikuwa imemwacha María Félix Nava akiwa hana njia ya kupokea marupurupu ya kujikimu kimaisha.
Baada ya taarifa kuhusu kisa hicho kuangaziwa na vyombo vya habari
Guadalajara, mmoja wa viongozi wa benki hiyo alijitokeza na akawasilisha hundi yeye binafsi kwa mwanamke huyo.
Sheria kuhusu uwazi hutaka marupurupu yote yalipwe kwa akaunti za benki za mnufaika.
Bi Félix alikaa miezi mitatu bila kupokea marupurupu baada ya kuzuiwa kufungua akaunti ya benki na tawi la benki ya Citinamex.
"Waliniambia umri wa juu zaidi ni miaka 110," alisema.

Marekani kuimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini

Taifa la Korea kaskazini limekuwa likitoa picha kuhusu zoezi la kijeshiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionTaifa la Korea kaskazini limekuwa likitoa picha kuhusu zoezi la kijeshi
Mamlaka ya rais Donald Trump imewaelezea maseneta wote 100 wa bunge la taifa hilo kuhusu tishio la Korea Kaskazini na kubaini mikakati ya kuishinikiza Pyongyang kupitia vikwazo vya kiuchumi na vile vya kidiplomasia.
Lengo ni kuilazimu Korea Kaskazini kusitisha mpango wa makombora ya masafa marefu pampja na ule wa Kinyuklia.
Mwandishi wa BBC mjini Washington anasema kuwa mkakati muhimu pia utakuwa kuirai China kuishinikiza Pyongyang.
Maseneta wa Marekani walielezwa na mamlaka ya rais Trump kuhusu tishio linaloletwa na Korea KaskaziniHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMaseneta wa Marekani walielezwa na mamlaka ya rais Trump kuhusu tishio linaloletwa na Korea Kaskazini
Seneta mmoja alisema kuwa habari hiyo kuhusu Korea Kaskazini ilikuwa muhimu sana.
Taarifa iliotolewa kwa niaba ya wizara ya Ulinzi na ile ya kigeni ilisema kuwa Marekani bado itaendelea na mazungumzo lakini imejiandaa kujitetea pamoja na washirika wake.

Majibu ya klabu ya Yanga kwa Dr Mwakyembe

Kumekuwa Na Mkanganyiko Wa Habari Na Upotoshwaji Wa Taarifa, Ambazo Si Sahihi Kuhusiana Na Yanga Kuchezesha
Kikosi Cha Pili Hapo Jana Dhidi Ya Kombaini Ya Majeshi Katika Uwanja Wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Naomba Kuliweka Jambo Hili Wazi Na Kuondoa Sintofahamu Zisizo Na Msingi Na Pengine Kufunga Mjadala Huu Rasmi.
1.Week End Ya Tarehe 22 Na 23 ,Na Ya 28 Hadi 30 Tff Walitupa Ratiba Ambayo Inaonyesha Hakuna Mchezo Wowote Local League,
Au Fa Cup.Na Ratiba Yetu Ilionyesha Tutacheza Tarehe 22 Fa Cup Dhidi Ya Prisons Tu Kwa Kuwa Ni Kiporo,Na Ukiangalia Ni Wiki Ya Pili Sasa Ligi Haichezwi Kutokana Na Ratiba Ya Chan Yaani Mashindano Ya Kimataifa Ya Caf Kwa Timu Za Taifa Kwa Wachezaji Wa Ndani.
2.Baada Ya Kupata Ratiba Ya Mapumziko Ya Wiki Mbili Bila Michezo Ya Ushindani ,Kama Viongozi Tukaona Si Busara Wachezaji Wakae Bila Michezo Ya Kujipima Nguvu Ili Kuendelea Kujijenga Kuwa Katika Ushindani Muda Wote.
Tukaona Wiki Mbili Ni Nyingi Mno Bora Tupate Michezo Ya Kujipima Nguvu Yaani Friends Matches Katika Majuma Haya Mawili.
Tulipokea Barua Kutoka Arusha Tucheze Mechi Mbili Tarehe 29 Na 30 Dhidi Ya Madini Na Afc,Tukakubaliana Nao Pia Tutaenda Huko.
Tukapokea Barua Ya Dodoma Tucheze Tarehe 26 Tukakubali Pia.
Sasa Tatizo Limekuja Kwa Tff Kufanya Droo Tarehe 23 ,Na Kututaka Tucheze Tarehe 30 Nusu Fainali Ya Fa Cup Ratiba Ambayo Haikuwepo Kabla Ya Hapo ,Sisi Tulikubali Kucheza Michezo Hiyo Tukijua Hakuna Mashindano Yoyote Ndani Ya Tarehe Hizo.
3.Nakiri Kabisa Kuwa Tatizo Limesababishwa Na Ratiba Zisizoeleweka Za Tff Tusingefika Hapo,
Kama Ratiba Ya Tff Ingekuwa Si Kukurupuka Tusingefika Hapo Leo.
Tumecheza Mechi Ya Kiporo Na Prisons Tukashinda Huku Tukiwa Na Majeruhi Wanane Key Players.
Vicent Bossou
Donald Ngoma
Haruna Niyonzima
Juma Abdul
Malimi Busungu
Ally Mustapha
Anthony Mateo
Deus Kaseke
Siku Ya Pili Ratiba Inatoka Tucheze Nusu Fainali,Narudia Tena Nusu Fainali Tucheze Ndani Ya Siku Saba.
Kwa Vyovyote Vile Hata Ingekuwa Vipi ,Kwa Kikosi Tegemezi Cha Wachezaji 18 Tu,Kukichu Kua Na Kwenda Kukipiganisha Katika Michezo Miwili Mfululizo Ambao Mmoja Hauna Tija Kabisa Tena Michezo Hiyo Ipishane Kwa Siku Tatu Tu, Hii Haijawahi Fanywa Na Timu Yoyote Duniani.
4.Kwa Kuliona Hilo Na Kwa Mapenzi Ya Dhati Kabisa Kutoka Mioyoni Mwetu Viongozi Dhidi Ya Wapenda Mpira Wote Wa Mkoa Wa Dodoma Na Maeneo Ya Jirani,Viongozi Kwa Pamoja Sote Tulitafakari Tukasema Kheri Ya Nusu Shari Kuliko Shari Yenyewe.
Kwa Pamoja Tukahamua Kupeleka Timu Ya Kikosi Cha Pili Wakichanganyika Na Wale Wa Kikosi Cha Kwanza Ambao Hawajatumika Muda Mrefu Waungane Na Vijana Hao Kwenda Kuwapa Burudani Wananchi Wa Kanda Ya Kati Dodoma.
5.Nashukuru Timu Ikiongozwa Na Mimi Mjumbe Mkemi,Mjumbe Hashimu Na Mjumbe Siza Imefika Salama Na Bado Ipo Salama Salmin Na Jana Imeonyesha Kiwango Cha Juu Kabisa Na Wale Waliokuwa Hawaamini Waliacha Viti Vyao Na Kushangilia Soka Safi Na Maridadi La Vijana Wa Yanga.
Mpaka Nikawatania Vijana Ni Hali Hii Wangekuja Baba Zao Ndiyo Msingekaa Vitini Muda Wote.
Kwa Machache Ni Hayo Ila Na Peleka Pongezi Kwa Benchi La Ufundi La Yanga B Chini Ya Kocha Shadrack Msajigwa Kwa Kiwango Bora Kabisa Cha Timu Yake Amewapika Vizuri Hakika Hiki Ni Kikosi Hadhina Maridhawa Ya Yanga Hapo Baadae.
Nitakuwa Mchoyo Wa Fadhila Kwa Pato Ngonyani Alikuwa Captain Jana Kiwango Kizuri Hakika Anarudi Sasa.
Yote Katika Mwisho Pongezi Kubwa, Nzuri Sifa Kedekedee Kwa Yusuf Mhilu Mfungaji Bao La Kusawazisha Dhidi Ya Majeshi,Siyo Sifa Hizi Kwa Ajili Ya Goli Tu La Hasha Hakuna Aliyekaa Bila Kutoa Yowe La Furaha Kila Aliposhika Mpira, Huyu Ni Messi Wa Tanzania Kwa Vizazi Vipya Vya Mpira Tanzania.
Mwisho Kabisa Naliomba Shirikisho La Mpira Tanzania (TFF), liwe Linatoa Kalenda Au Ratiba Ambazo Baadae Hazitaleta Mitafaruku Kama Hii Hapo Baadae .
Yanga Oyeee
Daima Mbele
Nyuma Mwiko
Salum Mkemi
Mjumbe Kamati Ya Utendaji Yanga.
Msimamizi Mkuu Wa Idara Ya Habari Na Mawasiliano Yanga.

WAPINZANI NCHINI KENYA WAMPA ODINGA

Raila Odinga
Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) umemteua aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka 2017.
Bw Odinga sasa atakabiliana na Rais Uhuru Kenyatta atakayetumia chama cha Jubilee kuwania muhula wa pili.
“Hii ni heshima kubwa sana ambayo ndugu zangu wamenifanyia, kwa kuniweka nipeperushe bendera ya NASA.Tumekuwa na vikao ambavyo vimechukua siku nyingi. Kila kitu tumeandika, tumekubaliana ya kwanza serikali tutakayoiunda, ambayo ni serikali ya mseto itakuwa ni serikali ya mpito,” alisema Bw Odinga akihutubu baada ya kutangazwa kuwa mgombea.
Amesema atakuwa kama Joshua kwenye Biblia na kuvusha Wakenya hadi nchi ya ahadi.
“Sisi tuko kama timu, yenye pembe tano (Pentagon), wamenipa utepe wa nahodha, hiyo inaniunganisha mimi nao na Wakenya wote, tutatembea pamoja bega kwa bega. Tunataka kubadilisha Kenya na kutekeleza ndoto ya waanzilishi wa taifa letu”.
Alisema serikali yake itaangazia kumaliza umasikini, kuimarisha afya, kuboresha uchumi, kubuni nafasi za kazi na kurejesha gharama ya elimu na maisha chini.
Bw Odinga pia ameahidi kuhakikisha walimu na madaktari,pamoja na wafanyakazi wengine wanalipwa mishahara mizuri.
Kadhalika, ameahidi akishinda serikali yake itamaliza rushwa serikalini.
Makamu wa rais wa zamani Musalia Mudavadi amesema viongozi wote wakuu wa muungano huo wamekubalina kumuunga mkono mgombea huyo mmoja.
“Tumekubali kwamba mpangilio huu wa uongozi ni mpangilio ambao tunataka ulinganishwe na Rasimu ya Bomas ambayo Wakenya walitaka, lakini haikuidhinishwa,” amesema.
Amesema mpango wao ni kuwa wadhifa wa kinara wa mawaziri na msaidizi wake, kama ilivyokuwa kwenye rasimu hiyo ya katiba.

MUSIC