MKUTANO wa mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA, Edward Lowassa, jana uliweka historia mkoani Arusha baada ya wafanyabiashara kuamua kusitisha huduma zao na kwenda kumsikiliza mgombea huyo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Viwanja vya Sinoni.
Uwanja huo ulianza kujaa asubuhi ambapo kivutio kikubwa kilikuwa kwa mwanasiasa mkongwe ambaye hivi karibuni alitangaza kujiondoa CCM, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.
Akihutubia mkutano huo, Mzee Kingunge alisema ipo haja ya wananchikumchagua Lowassa awe Rais wa Awamu ya Tano ili aweze kuwaletea mabadiliko wanayoyahitaji.
Alisema Lowassa ana uwezo mkubwa wa kubadili maisha ya wananchina Tanzania kwa ujumla tofauti na CCM ambayo viongozi, wagombeawake hutumia muda mwingi majukwaani kuwashambulia wapinzani.
"Viongozi wa CCM wamesahau kauli ya hayati Mwalimu Nyerere aliposema watu wakikosa mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta njeya chama hicho; hivyo mchagueni Lowassa anatosha," alisema.
Aliongeza kuwa, viongozi wa CCM badala ya kunadi sera za chama chao, wanatumia majukwaa kutukana.
"Baada ya siku nne kuanzia leo, nitatoa siri nzito za CCM, nawaomba Watanzania msidanganyike na kitu chochote, CCM si chama bora, angalieni sera za Lowassa," alisema Mzee Kingunge.
Naye Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, James Mbatia, alisema watu wanaoambiwa mgombea urais wa CCM, Dkt. John Magufuli ndiyeanayefaa kuwa rais wanadanganywa.
Alisema mgombea huyo hana sifa za kuwa rais kama inavyodaiwa kwani utendaji kazi wake hauwezi kufanana na ule wa Lowassa.
Lowassa akerwa na umaskini.
Kwa upande wake, Lowassa alisema anakerwa na umaskini mkubwa walionao Watanzania; hivyo aliwaomba wamwamini kwa kumpigia kura za kutosha ili Serikali ambayo ataiunda iweze kukata kiu yao.
"Mlo mmoja wanaokula Watanzania utabaki kuwa historia, nataka kila Mtanzania ale milo mitatu kwa siku...nashangazwa na CCM inaposema itaboresha maisha ya Watanzania wakati uwezo huo hawana.
"Watanzania wengi wanateseka kutokana na ugumu wa maisha, hatakupata mlo mmoja ni shida...nauchukia umaskini, nikiingia Ikulu nitahakikisha sekta zote zinapiga hatua ya maendeleo," alisema.
Aliongeza kuwa, inashangaza kuona baadhi ya watoto wanakosa elimu, nchi ina rasilimali za kutosha kama madini, hifadhi za wanyama na gesi ambazo zinatosha kufuta umaskini.
"Mtoto wa Serikali ya Lowassa lazima asome hadi Chuo Kikuu bure, hikini kipaumbele changu, nipeni kura niwatumikie na kumaliza kero zenu mbalimbali zilizoshindwa kupatiwa ufumbuzi," alisema.
No comments:
Post a Comment