Kikao cha Ushauri cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Mara kimezikataa taarifa za mapato na matumizi za Wakala wa Serikali wa Umeme na Ufundi TEMESA na Hifadhi Ya Taifa ya Serengeti kwa madai ya kutokuwepo wawakilishi wa Idara hizo ndani ya kikao hicho.
Wajumbe wamefikia maamuzi hayo baada ya Mwenyekiti wa kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Butiama Annarose Nyamubi kuzitaka Idara hizo kuwasilisha Bajeti zao na kukosekana wahusika bila taarifa.
Katika Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Mara,kimezikataa Taarifa za Idara mbili za Temesa na Hifadhi ya Serengeti zilizopo Mkoani Humo,Kwa kile kinachodaiwa kukosekana kwa Washiriki Wa kuwasilisha Taarifa za Idara hizo Katika kikao hicho.
Wakizungumza Wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara,Wamesema kuwa kutokuwepo kwa Takwimu sahihi juu ya matumizi na mapato ndiyo chanzo cha kukataliwa kwa Bajeti hizo.
Akiwasilisha taarifa ya Wakala wa serikali wa umeme na ufundi Mhandisi wa Sekritariet ya mkoa wa Mara,Inginia Faustin Tarai Amesema kuwa kivuko cha Mv Musoma Kinaendelea na kazi zake japo kinakabiliwa na Kujaa maji eneo la kupandia Kivuko.
Kivuko Cha Mv Musoma kilicho chini ya TEMESA Kinakabiliwa na Tatizo la Abiria Kushindwa Kupanda Kivuko Hicho kutokana na eneo litumikalo na abiria kujaa maji na kusababisha Abria Kukanyaga maji ili kukifikia kivuko hicho.
No comments:
Post a Comment