Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mfanyabiashara maarufu Bongo, Emmanuel Mbasha
MWIMBAJI wa nyimbo za Injili na mfanyabiashara maarufu Bongo, Emmanuel
Mbasha amepotezea kuzungumzia suala la kumpa talaka mkewe kwa madai
kwamba yupo bize na suala la sherehe za ushindi wa rais Dk. John Pombe
Joseph Magufuli.
Aliyekuwa mke wa Emmanuel Mbasha, Flora Mbasha
Mbasha aliitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati mwanahabari wetu
alipomuuliza mwimbaji huyo kuhusu hatma ya kutoa talaka ambayo aliyekuwa
mkewe, mwimbaji Flora Mbasha amekuwa akiidai hadi kumfikisha
mahakamani.
Emmanuel Mbasha na mkewe
“Sikia bwana, mimi kwa sasa nipo bize na sherehe za ushindi wa Magufuli
siwezi kupoteza muda wangu kuzungumzia vitu vidogovidogo kama hivyo,
kwangu mimi rais wa nchi ni muhimu kuliko hayo mambo ya Flora
unayoniulizia,” alisema Mbasha.
Emmanuel na Flora walikuwa wanandoa na kubarikiwa kupata mtoto mmoja
kisha kugombana na kufikia hatua ya kuachana na sasa kila mmoja anaishi
kivyake.
No comments:
Post a Comment