Thursday, September 10, 2015

IS yateka kambi ya wanahewa wa Syria

Image copyrightAFP
Image captionIS yateka kambi ya wanahewa Syria
Ripoti kutoka nchini Syria zinasema kuwa kambi moja ya jeshi la wanahewa kaskazini mwa nchi imetekwa na wanamgambo wa Islamic state.
Kambi hiyo ilikuwa imezungukwa kwa kipindi cha miaka miwili.
Runinga ya taifa nchini Syria inasema kuwa wanajeshi waliondoka katika kambi ya Abu Duhur iliyoko kwenye mkoa wa Idlib.
Image copyrightReuters
Image captionWanajeshi hao waliondoka baada ya mashambulizo ya kila mara kutoka kwa kundi la Nusra Front
Wanajeshi hao waliondoka baada ya mashambulizo ya kila mara kutoka kwa kundi la Nusra Front lenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda.
Kambi hiyo ilikuwa kituo cha mwisho kilichokuwa kikidhibitiwa na serikali katika mkoa wa Idlib.

No comments:

MUSIC