Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na muungano wa UKAWA, ameutikisa mji wa Kahama kwa kuwa na rekodi ya kuwa na mafuriko ya watu katika mkutano wake wakuomba ridhaa yakupewa kura kwa ajili ya kuwaongoza wananchi.
Wakati akinadi sera zake Mh.Lowasa amesema kuwa iwapo akipata ridhaa yakuwa rais ataifanya Kahama Kuwa Mkoa kwani kwa ukubwa wake na wingi wa watu inajitosheleza.katika mwendelezo wake ameendelea kunadi sera yake ya ELIMU YA BURE kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu.
Wakati huo huo aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Bw.Mgeja ambaye walikuwa na ugomvi na Lembeli aliyekuwa mbunge wa Kahama kupitia CCM ambao wote sasa wamehamia CHADEMA amesema kuwa hawana tena ugomvi wataendelea kupambana kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa taifa.
MATUKIO KATIKA PICHA
No comments:
Post a Comment