Wednesday, April 26, 2017

Mbao FC yatangaza kiama kwa Yanga SC

Katika kuelekea hatua ya Nusu Fainali za michuano kombe la Shirikisho (FA), timu ya Mbao FC imeanza kujitapa kwa kusema wapo tayari kwa kuwapokonya ubingwa wapinzani wao Yanga SC siku ya Jumapili huku wakisisitiza kuwa Msuva na Tambwe kuwadhibiti.

Msemaji wa Klabu hiyo, Chrisant Malinzi amesema walikuwa na hamu kubwa ya kukutana na Yanga kwenye FA na kudai wamejiandaa ipasavyo katika safu yao ya ulinzi ambayo wanaamini ndiyo itaweza kuwapa upinzani mkubwa kwa washambuliaji hao.
Tulianza mipango yetu siku nyingi ya kujiandaa katika michuano ya kombe la FA na tulikuwa tukisubiria tu timu ya kupangwa nayo, tulikuwa na kiu ya kucheza na Yanga....Hatuhofii safu ya ushambuliaji ya Yanga kwani na sisi tuna safu nzuri ya ulinzi ya kuweza kuwazuia Msuva na Tambwe, tumejipanga vyema kuhakikisha tunapata nafasi ya kuingia fainali... Lengo letu ni kuona tunafanikiwa kutwaa taji ili kuwakilisha nchi kimataifa". Alisema Malinzi
Pamoja na hayo, timu ya Mbao FC ndiyo itakuwa wenyeji wa mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa alasiri mwishoni mwa Jumaa hili katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

No comments:

MUSIC