Monday, April 17, 2017

MAREKANI YATO KAULI NZITO KUHUSU KOREA KASKAZINI,,,

Bw Pence (kati) alitazama Korea Kaskazini kutoka kijiji cha mpakani Panmunjom 17 Aprili 2017.Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionBw Pence (kati) alitazama Korea Kaskazini kutoka kijiji cha mpakani Panmunjom
Bw Pence alisema hayo alipozuru eneo ambalo haliruhusiwi kuwa na wanajeshi katika mpaka wa Korea Kaskazini na Korea Kusini.
Ziara yake imetokea kipindi ambacho hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katika rasi ya Korea, huku Marekani na Korea Kaskazini zikijibizana vikali.
Bw Pence aliwasili mjini Seoul Jumapili saa chache baada ya Korea Kaskazini kutekeleza jaribio la kurusha kombora, ambalo halikufanikiwa.
Jumatatu, Marekani na Korea Kusini zilianzisha mazoezi ya pamoja ya majeshi yake ya wanahewa, kuhakikisha kwamba wanajeshi wake wako tayari kwa tishio lolote kutoka kwa Korea Kaskazini, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Korea Kusini.

Bw Pence, ambaye babake alipigana katika Vita vya Korea, alikuwa akihutubu katika kijiji cha Panmunjom siku ya Jumatatu.

No comments:

MUSIC