Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa adhabu ya faini ya Sh125 milioni kwa kampuni tano za simu za mkononi kwa kushindwa kuweka mazingira salama kwa wateja wao.
Kampuni hizo Airtel, Tigo, Smart, Halotel na Zantel, kila moja inatakiwa kulipa faini hiyo kabla ya Januari 29, mwakani.
Akitoa ufafanuzi wa adhabu hiyo jana, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Ally Simba alisema imetolewa kwa sababu kampuni hizo zimeshindwa kutimiza matakwa ya Kanuni za Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta ya mwaka 2011.
Sababu nyingine aliitaja kuwa ni kupuuza na kukaidi kufuata maagizo ya mamlaka iliyowapa Oktoba 16, mwaka huu kwa ajili ya kushughulikia matatizo hay
No comments:
Post a Comment