Waziri Mkuu Majaliwa alitoa msimamo huo jana bungeni wakati akijibu swali
la Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni.
Mbowe aliitaka serikali kuomba msaada wa Scotland Yard kuchunguza
kupotea kwa Sanane.
Mbali na tukio hilo, Mbowe alitaka taasisi hiyo pia ichunguze matukio ya
utekaji watu na kuuawa kwa askari polisi mara kwa mara katika mkoa wa
Pwani.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Boaz
aliiambia Nipashe mwezi mmoja uliopita kuwa ofisi yake haikuwa imefanikiwa
kupata taarifa za kilichompata Saanane.
Sanane alipotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba mwaka jana.
Majaliwa alisema serikali haiwezi kualika kikosi hicho cha polisi wa malkia wa
Uingereza kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini vina uwezo mkubwa wa
kuchunguza matukio ya uhalifu yanayotokea.
Aidha, Majaliwa alisema matukio ya utekaji na mauaji ya polisi yaliyotokea vyombo vya
ulinzi na usalama bado vinaendelea na uchunguzi na pindi utakapokamilika taarifa
itatolewa.
Mbowe alisema ni miezi sita sasa imepita tangu kupotea kwa msaidizi wake huyo na
hakuna taarifa yoyote ya serikali kuhusu tukio hilo.
Alisema hivi sasa taifa lina hofu, Watanzania wana hofu ya kikatiba na pia watu wanapotea
ovyo hali inayosababisha hofu zaidi kwa Watanzania.
Mbowe alisema Serikali inapaswa kuomba msaada wa kiuchunguzi kama ilivyowahi
kufanywa na Kenya alipouawa kiongozi wa juu wa serikali, Robert Auko, katika mazingira
ya kutatanisha. Alisema waliomba msaada katika taasisi hiyo ya Uingereza kuja
kuchunguza.
No comments:
Post a Comment