Thursday, April 27, 2017

Atakaye vunja Muungano atavunjika yeye - Magufuli

 
Rais Dk. John Pombe Magufuli, leo amewaongoza Watanzania katika maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais Dk. John Pombe Magufuli, leo amewaongoza Watanzania katika maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na Hayati Mwalimu Julias Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Abeid Aman Karume mwaka 1964.
Wakati akihotubia Rais Dokt. John Magufuli amewasii watanzania kuendelea kudumisha na kuimarisha Muungano baina ya Tanzania na Zanzibar ulijengwa na waasisi wa taifa hili huku akisisitiza kuwa atakayethubutu kujaribu kuvunja Muungano huo atavunjika yeye.
Rais Magufuli ameyasema hayo pindi alipokuwa anahutubia wananchi katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za Muungano zilizofanyika kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma kwa kusema kila mtanzania anaowajibu wa kulinda Muungano uliopo na kusisitiza kwamba njia pekee ya kuulinda ni kuchapa kazi kwa bidii.
"Mimi na mwenzangu Dkt. Shein tutafuta nyayo za wenzetu waliotutangulia kulinda Muungano huu kwa nguvu zote.... Asitoke mtu yoyote akajaribu kutaka kuuvunja Muungano wetu maana atavunjika yeye". Alisema Rais Magufuli
Pamoja na hayo, Rais Magufuli amesema kupitia Muungano kuna mafanikio mengi yamepatikana kutoka na juhudi za viongozi wa taifa na waasisi wa Muungano huo huku akipiga kijembe kwa kusema 'ukiona vyaelea ujue vimeundwa'

No comments:

MUSIC