Ukosefu wa maji ya uhakika katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga unadaiwa kuzorotesha huduma za tiba kwenye Hospitali ya wilaya hiyo iliyoanza kutoa huduma novemba mwaka jana na kupewa jina la dokta Jakaya Kikwete
Hali hiyo imebainika wakati wa shirika la Good Neighbos lilipokuwa linakabidhi msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya milioni 220 kwa ajili ya Hospitali ya wilaya ya Kishapu
Ni wakazi takribani laki tatu wakitegemea matibabu kutoka katika Hospitali ya wilaya ya Jakaya Kikwete Kishapu lakini changamoto iliyopo kwenye hospitali hiyo ni uhaba wa maji na kusababisha huduma kuzolota
Mkuu wa wilaya Bi Hawa Nghumbi na mganga mfawidhi wa Hospitali Gong Homa Henry wamesema maji katika wilaya hiyo pamoja na Hospitali imekuwa ni changamoto kubwa kwa wakazi wake.
Hata hivyo pamoja na changamoto hiyo shirika lisilokuwa la kiselikali la Good Neighbor kupitia kwa mkurugenzi wake Inseok Lee wametoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya milioni 220
Hospitali ya Dk Kikwete ina watumishi 37 wa kada mbalimbali wakati upungufu watumishi 163.

No comments:
Post a Comment