Waziri
Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye mchana huu anatarajiwa kujiunga na Chama
Cha NCCR-Mageuzi katika kile kinachoitwa "Mpango Mbadala" kutokana imani
ya viongozi wa UKAWA kwamba lolote litatokea kwa Mgombea wa UKAWA
kutokana na hali yake ya afya kuendelea kutetereka kwa kasi.Mazungumzo kati ya UKAWA na Bwana Sumaye yamechukua uharaka mpya hivi karibuni kutokana na ukweli kwamba katika kipindi hiki kifupi
ambacho viongozi wa UKAWA wamekuwa karibu na Bwana Lowassa ndipo wameshuhudia ukubwa wa tatizo lake la afya na katika vikao ambavyo havikumhusisha Lowassa wamejiridhisha kwamba hataweza kufanya kampeni nchi nzima kwa ufanisi na kwamba, hata kama wakishinda uchaguzi, Bwana Lowassa hatakuwa na uwezo wa kuendesha Serikali.
Aliyeongoza mazungumzo ya kumshawishi Bwana Sumaye ni Bwana James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, Askofu Sendoro wa KKKT, Mchungaji Mtaita. Askofu Stephen Munga wa KKKT pia alihusika kwa nyakati tofauti. Bwana Sumaye, ambaye amekuwa hasimu mkubwa wa Bwana Lowassa, alishawishiwa kwa hoja tano:
Viongozi wa UKAWA walimshawishi Bana Sumaye kwamba wana nafasi ya kushinda lakini wana uhakika kwamba Bwana Lowassa hatakuwa na nguvu, afya na uwezo wa kuendesha Serikali kwahiyo yeye, kwa utaratibu mahsusi, ndiye atakayeendesha Serikali. Lakini pia walimshawishi kwamba litakapotokea lolote kwa Bwana Lowassa yeye ndio atakuwa Mgombea wa UKAWA.
Pia Bwana Sumaye alishawishiwa kwamba maisha yake yatatazamwa na hatakuwa na matatizo tena ya kifedha. Aliyechukua jukumu la kumlipa Bwana Sumaye kwasasa na baadaye kumtengenezea uchumi ni Bwana Anselm Minja, Mfanyabiashara wa Arusha.
Baada ya kuijulisha familia yake, taharuki imezuka huku familia nzima ikipinga suala hili la kuhamia UKAWA. Familia ya Sumaye ilikuwa na hoja tatu,
Kwanza: heshima ya Sumaye, ambaye sifa yake kubwa ni msimamo, itashuka kutokana na ukweli kwamba kwa miaka yote amekuwa akimsema Lowassa kwamba ni fisadi na aliwahi kutamka kwamba Lowassa akipitishwa na CCM yeye anaenda UKAWA. Sasa leo yeye ndiye anamfuata Lowassa alipo kwasababu ya madaraka.
Hoja ya pili ya familia ni hofu ya kitakachotokea pale UKAWA itakaposhindwa uchaguzi. Familia inakumbuka jinsi Sumaye alivyoporomoka kisiasa mara baada ya kushindwa mwaka 2005 na inakumbuka zaidi jinsi alivyodhalilika baada ya kushindwa kwenye U-NEC wa CCM na Mary Nagu kwamba 2012.
Familia inaamini kwamba wakati wa Sumaye kisiasa nchini umeshapita na Kwa kujiingiza kwake kwenye upinzani anaharibia wanae ambao wana maisha mbele zaidi.
Source. www.williammalecela.com
No comments:
Post a Comment