
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha uvumi ulioenea sehemu mbalimbali
kuwa Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama hicho,Dkt.John Pombe
Magufuli amewaahidi Walimu kuwapa Kompyuta kama CCM itapita madarakani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya
Chama hicho,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kauli
hiyo siyo ya kweli na haikutolewa na Mgombea huyo wa Urais,Dkt.Magufuli.
Hatahivyo,Nape amesema kauli hiyo imetolewa kwa nia mbaya kuonyesha Chama cha Mapinduzi kimeanza ziara ya kampeni mapema.
Amesema watu walioinukuu kauli hiyo wamesema imetoka katika Ilani ya
Uchaguzi ya Chama hicho,Nape amesema " Ilani ya Uchaguzi ya CCM imetoka
jana Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama uliofanyika jana mjini
Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23,mwaka huu katika uzinduzi wa
Kampeni,hivyo kauli yoyote iliyotoka kwa chama hicho ikidaiwa imetoka
katika Ilani yetu ya Uchaguzi,hiyo siyo ya kweli,kwani Ilani hiyo
itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni Agosti 23" alisema na Nape
kwa msisitizo.
Kuhusu msimamo wa Chama cha Mapinduzi kwa wanachama wanaohama chama
hicho,Nape amesema wanachama hao wanahama kwa mapenzi yao binafsi
wengine wamehama kwa sababu ya kushindwa katika kura za maoni za chama
No comments:
Post a Comment