Showing posts with label Games. Show all posts
Showing posts with label Games. Show all posts
Monday, November 9, 2015
Sunday, August 23, 2015
KUMEKUCHAA...JIONE HII NI BALAA
NI kweli kumekucha!
Kipyenga cha kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu 2015 kimepulizwa. Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema leo ndiyo siku ambayo wagombea
udiwani, ubunge na urais wa vyama vyote wanaruhusiwa kuanza kujinadi kwa
wapigakura, Risasi Jumamosilina kila kitu.
Jiji la Dar es Salaam ambalo linaaminika kuwa na wapiga kura wengi
kuliko majiji mengine manne nchini kote (Arusha, Mwanza, Tanga na
Mbeya), hali ni ya msisimko tangu juzi (Ijumaa) ambapo baadhi ya
barabara zilianza kuwekwa sawa kwa ajili ya kuruhusu wagombea kupita na
magari yao kwenda kwenye viwanja vya kampeni.
CCM, UKAWA NDIYO GUMZO
Kampeni jijini Dar zinazotazamwa kwa macho makubwa ni mbili. Ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM, mgombea wake John Magufuli) ambayo itasimamisha jiji
kesho kwenye Viwanja vya Jangwani vilivyopo wilayani Ilala na ile ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema, mgombea wake Edward Lowassa)
chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) zitakazofanyika Agosti 29,
2015 huku vyama vingine navyo vikianza leo nchini kote.
BARABARA YA MOROGORO
Mhandisi mmoja wa Halmashauri ya Jiji la Dar ambaye alisema yeye si
msemaji mkuu, alilidokeza gazeti hili kwamba, upande mmoja wa Barabara
ya Morogoro (kutokea Kariakoo kwenda Mbezi) utakula kitanzi kuanzia
mchana wa kesho ili kuwezesha magari ya msafara wa wana CCM, mgombea
wake, John Magufuli na wapambe kuweza kuingia kwenye viwanja hivyo kwa
ajili ya kuzindua kampeni ambayo rais anayemaliza muda wake, Jakaya
Kikwete ‘JK’ atakuwepo.
WASIO NA KAZI MUHIMU MJINI
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar ambao kesho watakuwa hawana kazi za
muhimu mjini, wametakiwa kujituliza majumbani mwao ili kukwepa usumbufu
unaoweza kujitokeza kutokana na usafiri wa umma kuingiliwa na misafara
ya kampeni, hususan kwa Barabara ya Morogoro.
Akitoa maelekezo kwa wakazi wa Jiji la Dar alipozungumza na wanahabari
ofisini kwake, Ilala juzi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky
Sadik alisema Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Suleimani Kova ataweka mambo yote hadharani.
KAMANDA KOVA
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, ni vyema wananchi wakatambua kuwa polisi
wamejipanga kuhakikisha ulinzi unakuwepo kwa asilimia mia moja.
“Polisi haitamuonea mtu. Ila nawaomba wale wanaotaka kutumia wingi wa
watu na misafara kufanya uhalifu waachane na mawazo hayo kwani jeshi la
polisi lipo macho saa ishirini na nne.”
Aidha, Kamanda Kova alipiga marufuku tabia za baadhi ya wakazi wa Jiji
la Dar kuwazomea wanachama waliovaa mavazi yenye utambulisho wa vyama
vyao.
CCM WATAMBA NA ‘HAPA NI KAZI TU’
Tayari wana-CCM wamekuwa wakiutumia msemo wa mgombea wao kwamba atafanya
kazi kwa kiwango cha juu ‘hapa ni kazi tu’ kujifagilia kwamba, ushindi
ni wao wakimpamba mgombea huyo kuibuka na ushindi wa kishindo.
UKAWA WAO NI ‘SAFARI YA MABADILIKO’
Wakati CCM, wakitamba na msemo wao huo uliojipatia umaarufu mkubwa
kwenye mitandao ya kijamii na mitaani, Ukawa wao wanasimamia ‘slogani’
ya Safari ya Mabadiliko ambayo mgombea wake, Edward Lowassa amekuwa
akiitumia tangu alipojiunga na umoja huo Julai, mwaka huu.
NI KAMA SIMBA NA YANGA
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar, walipozungumza na gazeti hili kuhusu
kuanza kwa kampeni nchi nzima leo, walisema ni kama refa amepuliza
kipyenga tayari kuanza kwa mpira wa fainali ya timu kubwa mbili za Simba
na Yanga.
Tuesday, April 28, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)